Jackie Matubia Aeleza Changamoto Alizopitia Katika Malezi ya Pamoja na Ex Wake

Jackie Matubia Aeleza Changamoto Alizopitia Katika Malezi ya Pamoja na Ex Wake

Muigizaji maarufu wa Kenya, Jackie Matubia, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu changamoto alizokumbana nazo alipokuwa akijaribu kulea mtoto kwa ushirikiano (co-parenting) na aliyekuwa mpenzi wake, Blessing Lung’aho. Akiwa mgeni kwenye G2G Podcast, Jackie alisema alijitahidi kwa dhati kuhakikisha kuwa mtoto wao analelewa katika mazingira ya upendo na ushirikiano, lakini juhudi zake hazikueleweka vyema na Lung’aho. “Nilijaribu, marafiki zake waliona. Nilikuwa namsogelea alipokuwa, hata kumtembelea, lakini alidhani nataka turudiane,” Jackie alieleza kwa hisia. Matubia alibainisha kuwa nia yake kuu ilikuwa kumpa mtoto wao nafasi ya kuwa karibu na wazazi wote wawili, licha ya uhusiano wao wa kimapenzi kuvunjika. Alisema kuwa alifanya jitihada nyingi kuhakikisha Blessing anahusishwa katika malezi, lakini mambo hayakuenda kama alivyotarajia. Hii ni mara ya kwanza kwa Jackie kuzungumza kwa uwazi kuhusu hali ya mahusiano yao baada ya kuachana, na kauli yake imeibua hisia mbalimbali miongoni mwa mashabiki wake na watumiaji wa mitandao ya kijamii. Wengi wamemsifia kwa ujasiri wa kuweka mbele maslahi ya mtoto wake licha ya changamoto za kibinafsi. Jackie Matubia na Blessing Lung’aho walikuwa wapenzi maarufu kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kutengana mwaka jana. Wawili hao walibarikiwa na mtoto mmoja katika kipindi cha uhusiano wao.

Read More