Msanii TID Alalamikia Kutolipwa Mirabaha na Kukosa Mikopo

Msanii TID Alalamikia Kutolipwa Mirabaha na Kukosa Mikopo

Msanii nguli wa muziki kutoka Tanzania, TID (Top In Dar), ameelezea masikitiko yake kuhusu changamoto zinazowakumba wasanii nchini humo, hasa kutolipwa mirabaha yao licha ya kazi zao kuendelea kutumika kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Kupitia mitandao ya kijamii, TID alisema kuwa licha ya wasanii kukosa fursa za mikopo na msaada wa kifedha, hata haki yao ya msingi ya kulipwa mirabaha kwa kazi wanazozalisha haitekelezwi. Alidai kuna zaidi ya shilingi bilioni moja zinazopaswa kuwalipa wasanii lakini hakuna uwazi kuhusu fedha hizo. Kwa mujibu wa TID, hali hiyo inaonyesha jinsi ambavyo wasanii, licha ya kuwa miongoni mwa watu wanaochangia sanaa, utamaduni, na uchumi wa taifa, bado wanakabiliwa na ukosefu wa heshima na uthamini kutoka kwa taasisi husika. “Mikopo Tumepigwa Chini Sawa…Basi hata hiyo MiRABAHA haki yetu nayo hatulipwi na Tunajua Kuna Zaidi ya 1 Bilioni sijui hapo tunakosea wapi sisi Wajenga Nchi wenye Vipaji,” Aliandika kupitia Instastory yake. Kauli yake imezua mjadala mpana kwenye mitandao ya kijamii, huku wapenzi wa muziki na wadau wa sanaa wakimtaka Waziri wa Utamaduni pamoja na taasisi za usimamizi wa mirabaha kutoa majibu kuhusu wapi fedha hizo zimekwama na kwa nini wasanii hawapati stahiki zao. TID ni miongoni mwa wasanii walioweka historia katika muziki wa Bongo Flava, na amekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wasanii wenzake kwa muda mrefu

Read More
 Harmonize Aendelea Kuumia Kimapenzi, Aandika Machungu Snapchat

Harmonize Aendelea Kuumia Kimapenzi, Aandika Machungu Snapchat

Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Harmonize, anaonekana kupitia kipindi kigumu upande wa mahusiano licha ya kuwa na jina kubwa kwenye tasnia ya muziki na utajiri wa kutosha. Kupitia akaunti yake ya Snapchat, Harmonize amemwaga hisia zake kwa uchungu kuhusu mpenzi wake ambaye bado hajawa tayari kumkubali kikamilifu kwenye maisha yake. Katika ujumbe wake, Harmonize alieleza kwa wazi kwamba ana mapenzi ya dhati kwa mwanamke huyo, na kwamba siku atakayokubali kuwa naye rasmi, atamuoa papo hapo bila kuchelewa. Hata hivyo, kwa sasa ameamua kumpa nafasi ya kuendelea na maisha yake huku yeye akiendelea kumsubiri kwa subira. “Mimi ni mtu mzima, niko tayari. Siku akiamua tu, sihitaji hata kupanga… nitamuoa siku hiyohiyo,” aliandika Harmonize kwa hisia kali. Mashabiki wengi wameonesha hisia tofauti, wengine wakimpongeza kwa uvumilivu na upendo wa kweli, huku wengine wakimshauri asijidhalilishe kwa mapenzi yasiyolipwa kwa kiwango sawa. Hii si mara ya kwanza kwa Harmonize kulalamika kuhusu changamoto za kimapenzi, jambo ambalo limezua mijadala mitandaoni kuhusu maisha ya mahusiano ya wasanii mashuhuri.

Read More
 Hanstone Aibua Madai Mazito Dhidi ya WCB Wasafi

Hanstone Aibua Madai Mazito Dhidi ya WCB Wasafi

Msanii wa Bongo Fleva, Hanstone, amevunja ukimya kuhusu maisha yake ndani ya lebo ya WCB Wasafi, akieleza hadharani changamoto alizokumbana nazo kipindi alichokuwa akihudumu humo. Akizungumza juzi kwenye mahojiano, Hanstone alidai kuwa alikaa ndani ya WCB kwa kipindi cha miaka mitatu bila kutambulishwa rasmi kama msanii wa lebo hiyo. Katika kipindi hicho, alieleza kuwa alihusika katika kuandika nyimbo kwa wasanii wengine, wakiwemo majina makubwa kama Diamond Platnumz, lakini hakuwahi kulipwa chochote kwa kazi hiyo.  “Nilitumika kuandika nyimbo kwa wasanii waliokuwa juu, lakini sikuwahi kupewa nafasi yangu wala stahiki zangu. Niliamini kwenye mchakato, lakini haikuwa kama nilivyotarajia,” alisema Hanstone kwa hisia. Kwa muda mrefu, mashabiki na wadau wa muziki wamekuwa wakimtaja Hanstone kama msanii asiye na subira, sifa ambayo imeonekana kuwa chanzo cha yeye kutopata nafasi ya kung’aa akiwa chini ya lebo hiyo ya WCB. Hata hivyo, msanii huyo amekana madai hayo, akisema alijitahidi kuwa mvumilivu, lakini hakupata fursa aliyostahili. Kauli ya Hanstone imezua mjadala mkubwa mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakionesha huruma na kumuunga mkono, wakati wengine wakihimiza wasanii chipukizi kuwa na uvumilivu zaidi wanapojiunga na lebo kubwa kama WCB. Kwa sasa, bado haijajulikana ikiwa Hanstone atachukua hatua za kisheria au ataendelea na muziki kama msanii huru nje ya lebo hiyo. Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona hatua yake inayofuata.

Read More
 Harmonize Atamani Kuwa Baba, Aonyesha Mradi Mkubwa wa Ujenzi

Harmonize Atamani Kuwa Baba, Aonyesha Mradi Mkubwa wa Ujenzi

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Harmonize, ameonesha hatua nyingine kubwa katika maisha yake ya kifedha na ya binafsi baada ya kuposti kwenye Instagram Story picha ya mjengo mkubwa unaoendelea kujengwa, ishara ya mafanikio na uthibitisho wa ndoto alizowahi kuzielezea huko nyuma. Picha hiyo, iliyopambwa na maneno “My future so bright, I need a son now”, imetoa ujumbe wenye maana pana: si tu kuhusu mafanikio ya sasa, bali pia taswira ya ndoto za baadaye. Harmonize anaonesha kuwa sasa anawaza si tu kuhusu kujenga majumba, bali pia kuanzisha familia na kupata mrithi wa jina lake. Kauli hiyo imeibua mijadala mitandaoni, wengi wakitafsiri kama ishara ya utulivu wa kisaikolojia na kifamilia, huku mashabiki wake wakimpongeza kwa hatua hiyo kubwa ya maisha. Wengine wamekuwa wakitaka kujua iwapo msanii huyo tayari ana mipango ya ndoa au mtoto kwa wakati huu. Harmonize, ambaye amepitia mengi katika maisha yake ya muziki na mahusiano, anaonekana sasa kuelekea kwenye ukurasa mpya unaochochewa na maono ya urithi, utulivu, na mafanikio ya muda mrefu.

Read More
 ERIC OMONDI AWATOLEA UVIVU WASANII TANZANIA, ADAI MUZIKI WA BONGOFLEVA UMEKUFA

ERIC OMONDI AWATOLEA UVIVU WASANII TANZANIA, ADAI MUZIKI WA BONGOFLEVA UMEKUFA

Baada ya kuuzungumzia sana muziki wa Kenya kiasi cha kukamatwa na polisi , akidai kuwa muziki Kenya unakufa na wasanii wake hawajitumi, mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi ameugeukia muziki wa Bongofleva na wasanii wake akidai muziki wa amapiano unaua utambulisho wa muziki wa Bongofleva kutoka Tanzania. Kupitia ukurasa wake wa Instagram mchekeshaji huyo mwenye zaidi ya wafuasi million 3.7 ameeleza kuwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki muziki wa bongofleva ndio ulikuwa kama utambulisho wa Ukanda huu lakini kwa kuiga muziki wa Amapiano ,muziki wa bongo fleva umepotea. Omondi amewataka wasanii wa Tanzania kuamka na kurudi katika utambulisho wao wa Bongofleva huku akidai kuwa wakenya wamelala , na inafaa watanzania warejee kwa upesi kwenye muziki wao kabla ya muda kuisha. EAST AFRICA I am SAD!!! I Weep for my PEOPLE😥😥😥. Nina Huzuni Moyoni😥. Bongo flava has always been East Africa’s PRIDE ila Kwa sasa IMEKUFAA. Kila Tanzania Artist Kwa sasa Anaimba Amapiano. We have lost our CULTURE, Killed our Own!!! Tumekaribisha, tumeiga, tumeichukua Tabia na Mwenendo zake Jirani tukajisahau wenyewe😥😥😥. We are LOSING OUR IDENTITY, OUR PRIDE!!! Naomba ndugu Zangu Wa BONGO Turejee kwa upesi before it’s too late!!! Wakenya WAMELALA, Wa Tanzania WAMEJIPOTEZAA. Mungu TUHURUMIE, TUREHEMU🙏🙏😥😥…aliandika Omondi kupitia Instagram yake

Read More