BOOMPLAY WAINGIA MKATABA NA TELKOM KENYA KURAHISISHA HUDUMA ZA KUSTREAM MUZIKI
Mtandao wa Boomplay umeingia ubia wa kufanya kazi na kampuni ya mawasiliano ya Telkom Kenya kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za kustream muziki miongoni mwa wakenya. Ushirikiano huo ambao utatoa nafasi kwa wakenya kupata huduma ya kupakua na kusikiliza muziki katika app ya Boomplay kwa urahisi, inakuja na vifurushi mbali mbali ambazo zitawezesha watumiaji wa telkom kusikiliza zaidi ya nyimbo millioni 75 za humu na kimataifa kwa shillingi 299 kwa mwezi. Vifurushi hivyo pia vitatoa fursa kwa watumiaji wa Telkom kusikiliza muziki usiokuwa na matangazo lakini pia kupakua muziki bila kikomo kutoka kwa wasanii kama Otile Brown, Khaligraph Jones, Nadia Mukami, Nikita Kering na wengine wengi. Packages zitakazozinduliwa ni pamoja na ya shilllingi 49 kwa siku, shillingi 159 kwa wiki na shilling 299 kwa mwezi, virushi ambavyo vitakuwa vinakata mjazo wa watumiaji wa Telkom.
Read More