WASANII WA BOONDOCKS GANG EXRAY NA ODI WA MURANG’A WAFUNGUKA KUHUSU HALI YA EDU MADOXX

WASANII WA BOONDOCKS GANG EXRAY NA ODI WA MURANG’A WAFUNGUKA KUHUSU HALI YA EDU MADOXX

Wasanii wa Boondocks gang, Exray na Odi wa Murang’a wamejibu tuhuma zilizoibuliwa na aliyekuwa member wa kundi hilo, Edu Maddox. Wakipiga stori na podcast ya Presenter Ali wasanii hao wamekanusha madai ya  kumtumia vibaya Madoxx huku wakisema kwamba msanii huyo alikuwa anapenda sana kuishi maisha ya starehe, kitendo ambacho kilimpelekea kushindwa na shughuli za muziki. Aidha wamesema kwamba walihamua kujitenga na madoxx kwa sababu alikuwa kizingiti kwa maendeleo ya kundi la Boondocks kimuziki. Hata hivyo wamepuzilia mbali madai ya kumzuia Maddox kufungua akaunti yake ya youtube kwa kusema kwamba kila msanii wa kundi la Boondocks ana akaunti ya youtube ila uzembe wake wa kutofanya kazi umemfanya kutoachia kazi zake kama msanii wa kujitegemea. Hata hivyo wamethibitisha kuwa bado kundi la boondocks lipo imara licha ya utofauti ambao mwanachama mwenzao Maddox aliibua kwenye mitandao ya kijamii ambapo wameahidi kumlipia gharama ya kumpeleka rehab. Kauli ya exray na Odi wa Murang’a inakuja mara baada ya madox kudai kuwa alijiondoa kwenye kundi la Boondocks Gang kwa sababu hakufaidi na chochote kimuziki kutokana na wasanii hao kumtenga kwenye shughuli zao za kimuziki.

Read More
 KUNDI LA MUZIKI WA GENGETONE, BOONDOCKS GANG LAVUNJIKA RASMI

KUNDI LA MUZIKI WA GENGETONE, BOONDOCKS GANG LAVUNJIKA RASMI

Msanii wa kundi la Boondocks Gang, Madoxx amethibitisha rasmi kuvunjika kwa kundi hilo ambalo lilikuwa linaundwa na wasanii Exray na Odi wa Muranga. Katika Mahojiano yake ya hivi karibuni na Presenter Ali, Madoxx amesema wasanii waliokuwa wanaunda kundi hilo Exray na Odi walianza kumtelekeza kwa kumu-unfollow kwenye mtandao wa Instagram mara baada ya kuachia wimbo wao wa mwisho uitwao Dhidhi miezi 6 iliyopita . Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba amekuwa akipitia manyanyaso kwenye suala la ufanyaji kazi katika kundi la Boondocks kwani kwa kipindi cha muda mrefu amekuwa akipewa verse za mwisho kwenye nyimbo zao ambazo wamekuwa wakiziachia. Maddox amedai kuwa uongozi wa Boondocks umekuwa na upendeleo kwa wasanii Exray na Odi wa Murang’a kwa kuwa walipewa ruhusa ya kufungua chaneli zao za mtandao wa youtube huku wakimbania kufungua chaneli yake binafsi ili aweze kuachia nyimbo zake kama msanii wa kujitegemea. Hata hivyo amesema hana ugomvi wowote na wasanii wenzake Exray na Odi wa Murang’a huku akikanusha kupata usaidizi kutoka kwa uongozi wa Boondocks baada ya taarifa yake kusambaa mtandaoni kuwa amefungiwa nyumba aliyokuwa akiishi kutokana na kushindwa kulipa kodi. Utakumbuka kundi la Boondocks Gang lilikuwa linaundwa na wasanii watatu Exray, Odi wa Murang’a na Maddox na lilipata umaarufu nchini mwaka wa 2019 kupitia muziki wenye mahadhi ya Gengetone.

Read More