Rapa kutoka Kenya Boutross aachia rasmi Album yake mpya

Rapa kutoka Kenya Boutross aachia rasmi Album yake mpya

Rapa kutoka nchini Kenya Boutross ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la Mawingu. Album hiyo yenye jumla ya nyimbo 9 za moto, ina kolabo 7 kutoka kwa wakali kama Trio Mio, Maandy, Juice Man, Young Kith, Savage, na Beevlings. Mawingu Album kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani na ina ngoma kama Dapa Dapa, Can’t Wait, Ithaa, Demand na nyingine nyingine. Hii ni Album ya tatu kwa mtu mzima Boutross tangu aanze safari yake ya muziki baada ya “Kabla ya Mtindo” iliyotoka mapema mwaka wa 2022 ikiwa na jumla ya mikwaju 8 ya moto.

Read More
 BOUTROSS AACHIA RASMI KABLA MTINDO EP

BOUTROSS AACHIA RASMI KABLA MTINDO EP

Hatimaye Rapa kutoka nchini Kenya Boutross ameachia rasmi EP yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake. Hitmaker huyo  wa ngoma ya “Yea Yea Yea” amewabarki mashabiki zake na  “Kabla Mtindo” , EP ambayo ina jumla ya nyimbo 8 za moto, ikiwa na kolabo 7 pekee kutoka kwa wakali kama Chinbees, Ndovu Kuu,Barack Jacuzzi, Munyax,na wengine wengi. EP hiyo kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani na ina ngoma kama Uchi Wale, Mwanangu,Sweety,  Confuse Me na nyingine nyingine. Hii ni EP ya tatu kwa mtu mzima Boutross, tangu aanze safari yake ya muziki baada ya 6IX ya mwaka wa 2019 na Billy Jean ya mwaka wa 2018. Lakini pia ana 6ixviewsii8k mixtape iliyotoka mwaka wa 2020 ikiwa na juma ya mikwaju ya 24 ya moto

Read More