Brazil yatupwa nje Kombe la Dunia

Brazil yatupwa nje Kombe la Dunia

Timu ya Taifa ya Croatia imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa kuiondosha Brazil kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya timu hizo kumaliza dakika 120 zikiwa sare ya 1-1 Brazil ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo kabla ya kukutana na kigingi cha Croatia walioendeleza kile walichokifanya kwenye fainali zilizopita walipovuka kwenye hatua zote za mtoano kwa kucheza dakika 120 kuanzia hatua ya 16 Bora hadi fainali walipofungwa na Ufaransa Mwaka huu Croatia imewatoa Japan katika hatua ya 16 Bora na sasa wamewaondosha Brazil kwa mbinu zile zile na watakutana Argentina kwenye nusu fainali Argentina ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa kuwaondosha Uholanzi kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya timu hizo kumaliza dakika 120 zikiwa sare ya 2-2

Read More
 Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil Neymar kukosa mechi mbili

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil Neymar kukosa mechi mbili

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil Neymar hatashiriki mechi mbili zijazo za Brazil za Kombe la Dunia (Switzerland & Cameroon) baada ya kupata jeraha sehemu ya fundo la mguu wa kulia, kwa mujibu wa taarifa toka kwa daktari wa timu yao. Mshambuliaji huyo aliondolewa uwanjani dakika ya 80 ya mchezo wa siku ya Alhamisi ambapo Brazil waliichapa Serbia 2-0 baada ya kukabiliwa vikali na Nikola Milenkovic. Hivyo Neymar anatarajiwa kurejea uwanjani katika hatua ya mtoano ikiwa Mabingwa hao mara 5 wa kombe la Dunia watafuzu kwenda hatua hiyo

Read More