MSANII WA BONGOFLEVA HARMONIZE AKANUSHA KUWA SINGLE
Baada ya kuchukua headlines siku ya jana kwa kuelezea kuwa hana mpenzi mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize ameibuka kukanusha taarifa hizo ambazo zilienea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram mkali huyo wa ngoma ya Teacher’ ameandika ujumbe wa kukanusha taarifa hizo ,huku akitaka kuheshimiwa akiambatanisha na emoji za kucheka, jambo ambalo limetafsiriwa kama alikuwa anatafuta kuongelewa (kiki) Januari 22 mwaka huu Harmonize aliibuka kupitia mfululizo wa post zake kwenye insta story yake kusema kuwa haamini kama yupo singo tena. Haikuishia hapo alienda mbali na kuandika ujumbe ambao uliohisiwa kumlenga moja kwa moja mchumba wake Briana kwa kusema tuonane nikifikisha umri wa miaka 35 labda nina umri wa miaka. Hata hivyo Harmonize walimwengu kwenye mitandao ya kijamii walihoji kuwa huenda penzi la mwanamuziki na C.E.O.wa KondeGang Harmonize na mpenzi wake mzungu raia wa Australia Briana limevunjika. Ikumbukwe kuwa penzi la Harmonize na Briana lilianza rasmi mwishoni mwa mwaka jana miezi kadhaa baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Fridah Kajala.
Read More