Bridget Blue aachia Rasmi Album yake mpya

Bridget Blue aachia Rasmi Album yake mpya

Msanii anayewakilisha Kenya kwenye tuzo za AFRIMMA 2022 Bridget Blue ameachia rasmi album yake mpya iitwayo “Colours” ambayo ina jumla ya ngoma 8. Album hiyo ambayo kwa sasa inapatikana kupitia majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani, haina collabo hata moja, kwani ngoma zote Bridget Blue kapita nazo mwenyewe. Album hiyo ambayo ilitayarishwa na prodyuza So Fresh 254 na nyimbo kama Window, Burnt, Ticking, Colours, Woman, Gimme your love, Times na Goodbye. Hii ni album ya kwanza kutoka kwa mtu mzima Bridget Blue chini lebo ya muziki ya Digit One Music.

Read More