Britney Spears Asema Aliwekewa Vizuwizi vya Kingono Wakati wa Uangalizi wa Kisheria
Malkia wa muziki wa pop, Britney Spears, ameibua hali ya sintofahamu mitandaoni baada ya kufichua madai ya kushtua kuhusu kile alichopitia wakati wa kipindi cha conservatorship (uangalizi wa sheria) kilichodumu kwa zaidi ya miaka 13. Kupitia chapisho kwenye mitandao ya kijamii, Britney alidai kwamba alilazimishwa kuvaa nguo za ndani zenye tabaka tatu ili kumzuia kufanya mapenzi, jambo ambalo limezua hisia kali na uvumi kwamba huenda alinyimwa uhuru wa msingi wa kibinadamu. “Walihakikisha sifanyi chochote. Hata kuwa na faragha kama mwanamke ilikuwa ndoto. Nililazimishwa kuvaa tabaka tatu za ‘tights’ ili nisiweze kushiriki tendo la ndoa,” aliandika Britney. Madai haya yamezua maswali mengi kuhusu namna alivyokuwa akitendewa wakati wa ule uangalizi wa sheria, uliokuwa ukisimamiwa na baba yake, Jamie Spears, pamoja na timu yake ya kisheria. Mashabiki na watetezi wa haki za binadamu wamelaani vikali kile kinachotajwa kama unyanyasaji wa hali ya juu dhidi ya mwanamke mtu mzima. Wafuasi wa harakati za #FreeBritney wameeleza masikitiko yao makubwa na kushinikiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina ili kuwawajibisha wote waliokuwa wakimnyanyasa msanii huyo. Hadi sasa, upande wa Jamie Spears haujatoa tamko rasmi kuhusu tuhuma hizi mpya. Hata hivyo, shinikizo kutoka kwa umma linaendelea kuongezeka, huku wengi wakisema ni wakati wa haki kutendeka.
Read More