Brown Mauzo Atangaza Kugombea Kiti cha MCA Kileleshwa 2027

Brown Mauzo Atangaza Kugombea Kiti cha MCA Kileleshwa 2027

Msanii Brown Mauzo, ametangaza rasmi kwamba atawania kiti cha Mjumbe wa Wadi (MCA) wa Kileleshwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Kupitia ujumbe wake kwa wakazi wa Kileleshwa, Mauzo amesema kuwa uamuzi wake umetokana na maombi na ushauri kutoka kwa jamii ambayo amekuwa akiishi nayo. Amesisitiza kuwa sauti ya wananchi wa Kileleshwa ndio imekuwa ikimpa motisha ya kuingia katika siasa. Mauzo ambaye pia ni mume wa zamani wa socialite Vera Sidika, ameongeza kuwa yuko tayari kushirikiana na wakazi wa Kileleshwa kubadilisha ward hiyo na kuboresha maisha ya watu. Hata hivyo, ameshukuru kwa imani na kuungwa mkono na wananchi, akiahidi kuendesha uongozi wa karibu na wananchi na unaolenga maendeleo.

Read More
 Brown Mauzo Akiri Bado Ana Hisia kwa Vera Sidika

Brown Mauzo Akiri Bado Ana Hisia kwa Vera Sidika

Penzi la Vera Sidika linaonekana kuendelea kumtesa msanii wa muziki Brown Mauzo, hii ni baada ya kukiri hadharani kwamba bado anampenda sosholaiti huyo licha ya kutengana kwao miezi kadhaa iliyopita. Mauzo amefunguka kupitia majibu kwa shabiki mmoja aliyemwandikia mtandaoni akisema walipendeza sana akiwa na Vera. Katika jibu lake, msanii huyo alikubali kuwa bado moyo wake haujamtoa Vera na kwamba anatamani kama wangeweza kurudiana. Kwa mujibu wa Mauzo, uhusiano wake na Vera haukuwa wa kawaida kwani ulimjengea familia na kumpa mtoto, jambo analolitaja kama kumbukumbu na baraka kubwa katika maisha yake. Ameeleza kwamba Vera ataendelea kubaki mtu wa kipekee moyoni mwake kwa sababu ya nafasi aliyopewa katika maisha yake. Uhusiano wa wawili hao uliwahi kuwa gumzo kubwa mitandaoni, uliojaa matukio ya kifahari, safari za kifamilia na hadithi za kimapenzi zilizoshirikishwa kwa mashabiki. Hata hivyo, baadaye walitangaza kuachana, kila mmoja akichukua mwelekeo tofauti. Vera alirudi kujikita katika biashara na maisha ya mitindo, huku Mauzo akijitahidi kurejea kwa nguvu kwenye muziki. Kauli yake ya sasa imeibua hisia mseto mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakimtia moyo kutafuta njia ya kusuluhisha tofauti zao na kumrudisha Vera, huku wengine wakimtaka akubaliane na hali na kuendelea mbele bila kumshikilia penzi la zamani.

Read More
 Brown Mauzo Aibua Mjadala Kuhusu Single Parents

Brown Mauzo Aibua Mjadala Kuhusu Single Parents

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Brown Mauzo, ameibua mjadala mtandaoni baada ya kueleza mshangao wake kuhusu ongezeko kubwa la wazazi wanaolea watoto pekee bila wenza. Kupitia hadithi zake za Instagram, Mauzo alionyesha kushangazwa na namna idadi ya single parents inavyozidi kupanda kila siku. Alisema hali hiyo imeibua swali kubwa kuhusu nani wa kulaumiwa katika changamoto hiyo, ikiwa ni wanaume au wanawake. Kauli hiyo imezua maoni tofauti mitandaoni, hasa ikizingatiwa kwamba Mauzo mwenyewe ana watoto na wake watatu tofauti (baby mamas). Wapo waliomuunga mkono wakiamini ametaja tatizo halisi la kijamii, huku wengine wakimshutumu wakidai historia yake binafsi inamnyima nafasi ya kutoa ushauri au maoni katika mjadala huo. Mjadala huu unaendelea kuibua maoni mseto kuhusu familia na malezi ya watoto, na unaonyesha jinsi suala la single parenting linavyoendelea kuchukua nafasi kubwa katika jamii ya sasa.

Read More
 Brown Mauzo Aweka Mipaka ya Simu Usiku kwa Wazazi Wenza

Brown Mauzo Aweka Mipaka ya Simu Usiku kwa Wazazi Wenza

Mwanamuziki wa Kenya Brown Mauzo ameweka wazi msimamo wake kuhusu mawasiliano katika mpangilio wa malezi ya pamoja (co-parenting), akisema hatakubali kupokea simu za usiku wa manane isipokuwa pale ambapo kuna dharura ya kweli. Kupitia ujumbe aliouchapisha mitandaoni, Mauzo ameeleza kuwa anathamini mipaka na utaratibu wa mawasiliano katika malezi ya watoto, akisisitiza umuhimu wa kuheshimiana kati ya wazazi wanaoshirikiana kulea. Mauzo, ambaye amekuwa akihusiana na mijadala ya malezi ya pamoja kwenye mitandao, amesema anataka kuhakikisha mawasiliano yanabaki ya heshima na yanafaa kwa maslahi ya watoto. Hata hivyo, haijabainika iwapo kauli hiyo ilimlenga Vera Sidika ila walimwengu mitandaoni wamehoji kuwa huenda kuna mgogoro ambao umeibuka kati yake na Baby Mama wake huyo ambaye kwa muda wamekuwa wakishirikiana kwenye safari ya ulezi wa pamoja. Kauli yake imezua mjadala miongoni mwa mashabiki na wafuasi, huku baadhi wakimuunga mkono kwa kuweka mipaka, na wengine wakihisi kuwa ujumbe huo ulilengwa kwa mtu maalum.

Read More
 Brown Mauzo avunja kimya chake kuhusu muonekano mpya wa Vera Sidika

Brown Mauzo avunja kimya chake kuhusu muonekano mpya wa Vera Sidika

Msanii Brown Mauzo amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya baby mama wake Vera Sidika kukiri kufanya upasuaji wa kupunguza makali yake kutokana na matatizo ya kiafya. Kupitia mtandao wa Instagram ameandika waraka mrefu akipongeza mrembo huyo kwa hatua ya kujitokeza wazi na kuweka mapungufu yake kwa umma huku akisema itakuwa funzo kwa wadada ambao kwa njia moja au nyinngine wataka kubadilisha miili yao kwa upasuaji. Katika hatua nyingine Mauzo amekiri kutamani maungo ya mrembo huyo kabla hajafanyiwa surgery ambapo ameenda mbali zaidu na kuhapa kwamba hatokuja kumkimbia Vera Sidika kutokana na muonekano wake mpya kwani alivutiwa na utu wake. Hata hivyo baadhi ya mashabiki wametafsiri ujumbe huo wa Brown Mauzo kuwa ni njia msanii huyo kutengeneza mazingira ya kuachia wimbo mpya huku wakienda mbali zaidi na kuhoji kuwa hatua vera sidika kutangaza hadharini kufanya upasuaji wa kupunguza makalio ilikuwa ni mkakati wa kumtoa kisanaa. Utakumbuka Brown mauzo na vera sidika ambaye walihalalisha mahusiano yao Septemba, 24 mwaka wa 2020 wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwae Amina Brown.

Read More
 BROWN MAUZO NA VERA SIDIKA MBIONI KUFUNGA NDOA

BROWN MAUZO NA VERA SIDIKA MBIONI KUFUNGA NDOA

Tutegemee ndoa kutoka kwenye couple ya mwanamuziki Brown mauzo na mrembo mwenye shape matata Vera Sidika mapema week ijayo. Hayo yamebainishwa kutoka kwa Instagram page ya mwanamuziki brown mauzo ambaye ameShare picha ya mrembo huyo na kuandika ujumbe unao ashiria kuwepo kwa ndoa kati yao huku akiweka wazi tarehe husika ya tukio hilo kuwa ni Januari 18 mwaka wa 2022. Hata hivyo walimwengu wameibuka kupitia mitandao ya kijamii na kuhoji kuwa brown mauzo anajianda kuachia kazi yake mpya ila anajaribu kutengeneza mazingira ili azungumziwe kwenye vyombo vya habari. Utakumbuka brown mauzo pamoja na vera sidika wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwae Amina Brown

Read More
 BROWN MAUZO AACHIA RASMI V ALBUM

BROWN MAUZO AACHIA RASMI V ALBUM

Mwanamuziki kutoka Kenya Brown Mauzo ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la V. V album imebeba jumla ya mikwaju 12 ya moto huku ikiwa na kolabo 5 pekee. Brown Mauzo amewashirikisha wasanii mbali mbali kama Masauti, Baraka the Prince,Ndovu Kuu, Mwasi, na Kaa La Moto. Kupitia ukurasa wake wa Instagram mauzo amesema ameachia album yake ya v kama zawadi kwa mke wake Vera Sidika ambaye juzi kati amejifungua mtoto wa kike aitwaye Princess Asia Brown. Album ya “V” ni album ya pili kwa mtu mzima Brown Mauzo baada ya Nitulize ya mwaka wa 2019. Hata hivyo Album hiyo inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya  kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Boomplay.

Read More
 VERA SIDIKA:NITAZAA KWA UPASUAJI

VERA SIDIKA:NITAZAA KWA UPASUAJI

Socialite  maarufu Afrika Mashariki Vera Sidika amesisitiza kwamba atajifungua kwa njia ya upasuaji na siyo kwa njia ya kawaida kwa sababu anaogopa uchungu wa leba. Vera ambaye anatarajia kujifungua muda wowote anasema kwamba, alifanya uamuzi kuwa atajifungua kwa njia ya upasuaji hata kabla hajapata ujauzito. Mrembo huyo ambaye anatarajia mtoto wake wa kwanza ameapa kwamba hakuna yeyote ambaye anaweza kubadilisha uamuzi wake. Mpenzi huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo amesema kwamba ni heri avumilie kipindi cha uponyaji baada ya kufanyiwa upasuaji kuliko akabiliane na machungu ya leba.

Read More