Bruno K Akanusha Tuhuma za Kusababisha Kifo cha Gogo Gloriose

Bruno K Akanusha Tuhuma za Kusababisha Kifo cha Gogo Gloriose

Msanii wa muziki kutoka Uganda, Bruno K, amekanusha vikali tuhuma za kusababisha kifo cha mwimbaji wa Injili kutoka Rwanda, Gogo Gloriose, aliyefariki dunia nchini Uganda tarehe 4 Septemba baada ya kuugua kwa muda mfupi. Bruno K amesema kuwa aliumizwa sana na madai ya baadhi ya wanablogu wa Uganda ambao walieneza uvumi kuwa alimfanyisha kazi kupita kiasi Gogo, jambo ambalo lilidaiwa kuchangia kifo chake, ili kumchafua mbele ya mashabiki wa Rwanda. Akipiga stori na Royal FM, amesema hatua ya kubebeshwa lawama kwa misingi ya uongo ni ya kikatili, akisisitiza kwamba lengo lake lilikuwa kumuinua Gogo kisanii na kumsaidia kupiga hatua katika muziki. Bruno K pia ameonyesha masikitiko yake kwa namna baadhi ya watu walivyopuuza kipaji cha marehemu wakati akiwa hai, lakini baada ya kifo chake wakaanza kuonyesha mapenzi makubwa kwake. Hata hivyo ametoa wito kwa mashabiki kuacha kupotoshwa na simulizi za uongo, badala yake waonyeshe mshikamano na familia ya Gogo katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Read More
 Msanii wa Uganda Bruno K Aanzisha Kampeini ya Kuchangia Mazishi ya Gogo Gloriose

Msanii wa Uganda Bruno K Aanzisha Kampeini ya Kuchangia Mazishi ya Gogo Gloriose

Mwanamuziki kutoka Uganda, Bruno K, ameanzisha kampeni ya kuchangisha fedha kusaidia mazishi ya msanii wa injili wa Rwanda, Gogo Gloriose, aliyefariki dunia nchini Uganda tarehe 4 Septemba baada ya kuugua kwa muda mfupi. Kupitia TikTok Live akiwa na meneja wa marehemu, Bruno K ameeleza kuwa kuna uhitaji wa dharura wa msaada wa kifedha ili kulipa bili ya hospitali na kuandaa usafirishaji wa mwili wa Gogo kurudi Rwanda kwa mazishi. Amesisitiza kuwa Gogo hakuja Uganda kwa shughuli za kibiashara bali alikuwa akihudumu, hivyo ni jukumu la mashabiki na makanisa aliyowahi kuhudumu kushirikiana kumpa heshima ya mwisho. Hata hivyo amebainisha pia kuwa mchango huo unahitajika kwa ajili ya kulipa bili ya hospitali, kununua jeneza na kugharamia gharama za usafirishaji wa mwili wake kuelekea Rwanda. Marehemu, kwa jina halisi Gloriose Musabyimanna, alikuwa amesafiri Uganda kuhudhuria ibada ya injili alipougua ghafla na kulazwa hospitalini Kyengera ambako alifariki dunia.

Read More
 Bruno K amjibu msanii Byg Ben kuhusu ukabila kwenye muziki Uganda

Bruno K amjibu msanii Byg Ben kuhusu ukabila kwenye muziki Uganda

Msanii Bruno K ametofautiana kimawazo na msanii chipukizi Byg Ben aliyedai kuwa ni vigumu kwa wasanii wasioimba nyimbo kwa lugha ya luganda kufanikiwa kisanaa nchini Uganda kutokana na ubaguzi wa kikabila uliokithiri nchini humo. Kupitia mitandao yake ya kijamii amemtaka msanii huyo kutia bidii kwenye kazi zake badala ya kutoa malalamiko yasiokuwa na msingi kwani mashabiki watamuunga mkono akitoa muziki mzuri. “Bro acha kutoa visingizio. Watu nchini Uganda watakuunga mkono bila kujali kabila lako. Wape tu muziki mzuri,” Bruno K aliandika Twitter.

Read More
 BRUNO K NA BINTIYE BRIELLA WALAMBA SHAVU LA UBALOZI IMPERIAL LEATHER UGANDA

BRUNO K NA BINTIYE BRIELLA WALAMBA SHAVU LA UBALOZI IMPERIAL LEATHER UGANDA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Bruno K pamoja na binti yake Briella wamelamba dili nono la ubalozi wa kampuni ya Imperial Leather. Bruno K amethibitisha taarifa hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kushare baadhi ya picha zikiwaonyesha wakitia sahihi mkataba wa maelewano na uongozi wa kampuni ya Imperial Leather. Hata hivyo mashabiki na mastaa mbali mbali nchini Uganda wameonekana kumpongeza Bruno K pamoja na mwanae Briella kwa mafanikio hayo makubwa maishani huku baadhi wakimponda msanii huyo kwa kumtumia vibaya binti yake kujipatia pesa wakati huu angali mdogo. Ikumbukwe mwezi mmoja uliopita Bruno K alimpoteza baby mama wake Rachel Nasasira baada ya kuagua kwa muda mrefu. Baada ya kifo chake kulikuwa na ripoti kuwa msanii huyo alikatazwa kumchukua binti yake Briella kutokana na hatua ya kumtelekeza baby mama wake akiwa hai. Lakini baadae alifanikiwa kumtorosha binti yake kutoka kwa mama ya mke wake kitu ambacho kiliibua mzozo mkali kati yake na familia ya baby mama wake wa wakimtuhumu kwa hatua ya kumrubuni mtoto huyo bila ya ridhaa yao.

Read More
 OSCAR ADAI BRUNO K ALIKIMBIA NA PESA ZOTE WALIZOPOKEA KUTOKA KWA WAHISANI

OSCAR ADAI BRUNO K ALIKIMBIA NA PESA ZOTE WALIZOPOKEA KUTOKA KWA WAHISANI

Siku chache  zilizopita msanii Bruno K alimtoa mwimbaji wa zamani wa Bigtym, Oscar kutoka kwenye lindi la umaskini. Hitmaker huyo wa Omulwa alimchuka msanii huyo na akaanza kumpa support, huku akiongoza kampeni ya kufufua kipaji  chake cha muziki ambacho kilikuwa kimefifia. Sasa  baada ya Oscar kupata afueni ameibuka na kumshutumu vikali Bruno K kwa madai ya kutogawa kwa usawa pesa walizopokea kutoka kwa wasamaria wema. Msanii huyo amehoji ni kwa nini Bruno K mwanzo alikuwa anajifanya anajali sana ilhali alikuwa na ajenda zake za kujinufaisha kupitia jina lake. Hata hivyo Oscar ametoa changamoto kwa Bruno k kuonyesha namna pesa walizopokea kutoka kwa waganda na makampuni mbalimbali ilivyotumika.

Read More