Kundi la BTS lachukua mapumziko hadi mwaka 2025

Kundi la BTS lachukua mapumziko hadi mwaka 2025

Kundi maarufu la Muziki toka Korea Kusini – BTS limetangaza kupumzika kufanya kazi kama Kundi hadi mwaka 2025. Kundi hilo liliundwa mwaka 2010 na kuanza kufanya vizuri mwaka 2013 ambapo katika kipindi hicho wamefanikiwa kupata mafanikio makubwa ikiwemo kushinda Tuzo kubwa mbali mbali na kutawala chart kubwa za Muziki duniani. Sababu ya kufikia maamuzi hayo ni kutaka kila mmoja afanye kazi binafsi (solo projects) lakini pia sababu nyingine kubwa ni kutimiza takwa la Kisheria ambapo baadhi ya memba watajiunga na mafunzo ya Kijeshi kwa mujibu wa sheria za nchi yao kuanzia Oktoba mwaka huu.

Read More
 KUNDI LA BTS LATANGAZA KUCHUKUA MAPUMZIKO KWENYE MUZIKI

KUNDI LA BTS LATANGAZA KUCHUKUA MAPUMZIKO KWENYE MUZIKI

Kundi maarufu la muziki kutoka Korea la BTS, limetangaza rasmi kuchukua mapumziko ya kazi kwa sasa kama kundi huku likieleza kila memba wa kundi hilo atafanya muziki kivyake. Kwenye taarifa yao kupitia channel yao ya youtube wameeleza watarudi baadae na kisha kuendelea na kazi za pamoja. Kundi hilo lenye mafanikio makubwa, linaloundwa na wasanii  7 ambao wamekuwa pamoja kwa takribani miaka tisa linaongozwa na RM, Jung Kook, V, Jimin, Suga, Jin na J-Hope. “Tutarudi upya na kufanya makubwa zaidi” – ameeleza Jung Kook. Hata hivyo hii inakuwa mara ya tatu kwa kundi hilo kutangaza kuchukua mapumziko, mara ya mwisho kutangaza hivyo ilikuwa ni mwaka 2019 na kisha baadae kurejea kwa kishindo.

Read More
 KUNDI LA BTS KUTOKA KOREA KUSINI KUPATA MAFUNZO YA KIJESHI MWAKA HUU

KUNDI LA BTS KUTOKA KOREA KUSINI KUPATA MAFUNZO YA KIJESHI MWAKA HUU

Members wa kundi maarufu la muziki duniani BTS maarufu kama Bangtan Boys kutoka Korean kusini kwa pamoja wanatarajiwa kujiunga na jeshi la nchi yao kupata mafunzo katika kipindi cha miezi 18 kama katiba na sheria ya nchi yao inavyo sema. Kundi hilo maarufu duniani linaloundwa na wanamuziki 7′ kwa pamoja wanatarajiwa kupata mafunzo hayo ndani ya mwaka huu 2022 ambayo ni ya lazima kwa kijana yoyote mwenye umri kati ya miaka 18 mpaka 27 aneyeishi korea kusini. Utakumbuka mwaka 2020 mchezaji nyota wa klabu ya Tottenham Hotspur ya ligi kuu nchini Uingereza Son Heungmin aliweza kushiriki mafunzo hayo na kupatiwa cheti na tuzo maalumu kuhitimu mafunzo.

Read More