STEFFLON DON ACHUKIZWA NA KAULI YA BURNA BOY,AMJIBU UMAARUFU NA PESA HUBADILISHA WATU

STEFFLON DON ACHUKIZWA NA KAULI YA BURNA BOY,AMJIBU UMAARUFU NA PESA HUBADILISHA WATU

Mwanamuziki kutoka Uingereza ambaye ni mpenzi wa msanii kutoka Nigeria Burna Boy, Stefflon Don amechukizwa na hatua ya Burna Boy kujitangaza kuwa hana mpenzi kupitia ukurasa wake wa Instagram. Kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Burna Boy aliandika ujumbe unaosomeka “Kwa taarifa yako, Odogwu hana mke.” Kauli hiyo ambayo iliamsha majibu ya wawili hao kuwa tayari wameachana, ilimuibua Stefflon Don ambaye alimrushia dongo Burna Boy kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kusema “Umaarufu na pesa hubadilisha baadhi ya watu” Mwimbaji huyo wa Uingereza alienda mbali zaidi na kusema, haijalishi ni kwa kiasi gani umemuonesha mtu upendo, uaminifu na vile umemfanyia mazuri, watu hujifanya wema kumbe ni feki tu. Stefflon Don na Burna Boy wameachana baada ya kuwa penzini kwa miaka mitatu.

Read More
 SAUTI SOL WAPOKEA CHETI CHA UTAMBUZI KUTOKA GRAMMY

SAUTI SOL WAPOKEA CHETI CHA UTAMBUZI KUTOKA GRAMMY

Kundi maarufu la muziki nchini, Sauti sol limepokea cheti cha utambuzi yaani (Certificate of Recognition) kutoka kwa waandaji wa tuzo za Grammy.   Cheti hicho ni maalum kwa ajili ya ushiriki wao kama watayarishaji kwenye album ya msanii Burna Boy kutoka Nigeria iitwayo “Twice As Tall” ambayo ilishinda tuzo ya Best Global Music Album kwenye tuzo za 63 za Grammy zilizofanyika mwezi wa tatu mwaka huu.   Sauti sol wameshiriki kwenye uandaaji wa wimbo namba 11 kutoka kwenye album ya “Twice As Tall” uitwao ‘Time Flies’.   Ikumbukwe, Sauti Sol kwa sasa wapo nchini Uingereza kwa ajili ya ziara yao ya kimuziki baada ya mapumziko ya takribani miaka miwili kutokana na janga la Corona.    

Read More