Butita Atoa Wito wa Umoja Katika Hafla za Kitamaduni za Waluya
Mchekeshaji, Eddie Butita, amesikitishwa na migawanyiko katika hafla za kitamaduni za jamii ya Waluya, akitoa wito kwa jamii hiyo kuungana na kuandaa tamasha moja kubwa badala ya kuwa na hafla nyingi zilizotawanyika. Akizungumza kupitia akaunti yake ya Instagram, Butita amehoji umuhimu wa kuwa na sherehe nyingi na kusema kwamba jamii hiyo haijawahi kuwa na tukio hata moja lililowahi kufanikiwa kutokana ukosefu wa umoja. Mchekeshaji huyo ambaye pia ni bosi wa SPM Buzz, amebainisha kuwa utengano wa hafla hizi unadhoofisha athari za kitamaduni za jamii, na kuwaleta watu pamoja chini ya sherehe moja kuu, kutatoa sauti yenye nguvu zaidi kwa utambulisho wa Waluya katika ngazi ya kitaifa. Aidha, Butita ametoa changamoto kwa promoters wa sherehe za kitamaduni kuchukulia jambo hilo kwa uzito na kuanza kupanga tukio moja kubwa litakalowakilisha jamii nzima. Watu wengi mitandaoni wameeleza kuwa hoja ya Butita inafungua mjadala kuhusu umuhimu wa kuunganisha tamaduni za Waluya na kuimarisha ushawishi wake katika masuala ya kitaifa.
Read More