Ombi la Kumtaka Gavana Newsom Kumsamehe Tory Lanez Lavuka Saini 250,000
Msanii maarufu wa muziki wa Hip Hop, Tory Lanez, ameendelea kupata uungwaji mkono mkubwa mtandaoni kupitia ombi lililowekwa kwenye mtandao wa Change.org, likimtaka Gavana wa California, Gavin Newsom, amsamehe. Kwa siku tatu mfululizo, ombi hilo limekuwa namba moja kwa kupendwa na kusainiwa zaidi kwenye jukwaa hilo, na kufikisha zaidi ya saini 250,000. Ombi hilo linataka msamaha rasmi kwa Tory Lanez kufuatia kifungo alichopokea baada ya kupatikana na hatia ya kumjeruhi rapa Megan Thee Stallion kwa risasi. Juhudi hizo zimeungwa mkono na watu maarufu kutoka tasnia ya burudani nchini Marekani, akiwemo Drake, Amber Rose, na Ty Dolla Sign. Wanaounga mkono ombi hilo wanadai kuwa hukumu dhidi ya Tory ilikuwa na upendeleo na kwamba anastahili kupewa nafasi ya pili. Hata hivyo, kuna kundi linalopinga hatua hiyo, likisema kuwa kila mtu anapaswa kuwajibika kwa matendo yake bila kujali umaarufu. Hadi kufikia sasa, ofisi ya Gavana Newsom haijatoa tamko rasmi kuhusu ombi hilo au uwezekano wa msamaha. Hali ikiendelea kuchacha, mjadala kuhusu haki, sheria, na nafasi ya watu maarufu mbele ya vyombo vya sheria unaendelea kushika kasi.
Read More