EDDY YAWE NA CAROL NANTONGO WAMALIZA TOFAUTI ZAO

EDDY YAWE NA CAROL NANTONGO WAMALIZA TOFAUTI ZAO

Carol Nantongo and msanii mkongwe nchini Uganda Eddy Yawe walitubariki na smash hit yao iitwayo “Tukigale” mwaka wa 2018. Wimbo huo ulifanya vizuri sokoni lakini wawili hao walikuja wakaiingia kwenye ugomvi kutokana na umiliki wake wa Tukigale kiasi cha kutotumbuiza wimbo huo kwenye matamasha mbali mbali ya muziki. Hata hivyo wikiendi hii iliyopita wawili hao walikutana jukwaani na wakatumbuiza pamoja wimbo wa Tukigale kwenye hafla moja ya harusi ambayo walialikwa kutoa burudani. Eddy Yawe na Carol Nantongo walionekana wakikumbatiana jukwaani kabla ya kuwaambia mashabiki zao kuwa wameweka tofauti zao kando kuhusu umiliki wa wimbo huo. Utakumbuka juzi kati Eddy Yawe walizozana na msanii mwenzake Martha mukisa baada ya kuachia kolabo yao itwayo Neteze.

Read More
 CAROL NANTONGO AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU BENDI YA MUZIKI YA GOLDEN

CAROL NANTONGO AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU BENDI YA MUZIKI YA GOLDEN

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Carol Nantongo amefunguka sababu iliyofanya kujiondoa kwenye bendi ya muziki ya Golden. Katika mahojiano yake hivi karibuni Carol Nantongo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ya “Oliwa” amesema bendi hiyo haikuwa na mazingira mazuri ya kufanyia muziki kwa sababu wanachama wake walianza kuchanganya kazi na siasa. Mwaka wa 2020 Carol Nantongo alijiondoa kwenye bendi ya Golden na akaanza kufanya muziki kama msanii wa kujitegemea. Golden Band ambayo ilikuwa chini Eagles Production ilikuwa inaundwa na wasanii kama Ronald Mayinja, Catherine Kusasira, Fred Sseruga, Stecia Mayanja na wengine wengi.

Read More