MULAMWAH ATISHIA KUMSHTAKI BABY MAMA WAKE CAROL SONNIE

MULAMWAH ATISHIA KUMSHTAKI BABY MAMA WAKE CAROL SONNIE

Mchekeshaji Mulamwah ametishia kumchukulia hatua kali za kisheria Baby Mama wake Carol Sonnie kwa hatua ya kumtumia vibaya mtoto wao mtandaoni. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Mulamwah ametoa ya moyo kwa kusema kuwa amechukizwa na kitendo cha Baby mama wake huyo kumtumia mtoto wao kama kitega uchumi, jambo ambalo amedai kuwa si cha kingwana kwani amekiuka haki ya faragha ya mtoto wao. Mchekeshi huyo ameenda mbali zaidi na kwa kudai kwamba kinachomuuma zaidi ni hatua ya mrembo huyo kumzushia madai ya uongo kwenye vyombo vya habari kuwa kuna kipindi alimshushia kichapo cha mbwa akiwa mja mzito, madai ambayo Mulamwah ameyakanusha vikali. Mapema wiki hii Mulamwah na Baby Mama Carol Sonnie walitupiana maneno makali mtandaoni kwenye kumbukizi ya kuzaliwa kwa mtoto wao baada ya mchekeshaji huyo kudai kuwa mzazi mwenzie amekuwa akimpa wakati mgumu kwenye suala la kutoa matunzo kwa binti yake.

Read More
 BABY MAMA WA MULAMWAH APIGA MNADA DREAD LOCKS ZAKE KWA KSHS. 300,000

BABY MAMA WA MULAMWAH APIGA MNADA DREAD LOCKS ZAKE KWA KSHS. 300,000

Baby Mama wa mchekeshaji Mulamwah, Carol Sonnie, ametangaza kupiga mnada na kuuza dread locks zake ambazo alinyoa juzi kati. Kwenye kikao cha maswali na majibu katika mtandao wa Instagram na mashabiki zake, Mrembo huyo amesema anauza nywele hizo kwa shilling laki 3 za Kenya na yeyote anayehitaji amtafute kwenye mitandao ya kijamii ili waweze kufanikisha mchakato wa manunuzi. Hata hivyo hatua hiyo imeonekana kuzua mjadala mzito miongioni mwa watumiaji wa mitandao wengi wakihoji huenda mrembo huyo atafuta mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni ikizingatiwa kuwa hakuna atakayenunua dread locks hizo hapa nchini. Kumbuka dread locks hizo ni za mwaka wa 2013 na Carol Sonnie amekuwa akizifanyia maboresho mara kwa mara licha ya watu kumshinikiza kuzinyoa.

Read More
 CAROL SONNIE AMJIBU KIMAFUMBO BABY DADDY WAKE MULAMWAH

CAROL SONNIE AMJIBU KIMAFUMBO BABY DADDY WAKE MULAMWAH

Baby Mama wa mchekeshaji Mulamwah, Carrol Sonnie amefunguka kwa mara ya kwanza siku chache baada ya Mulamwah kuibua kashfa nzito dhidi yake. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram ameandika ujumbe wa mafumbo ambao umetafsiriwa  na walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kuwa inamlenga moja kwa moja mpenzi wake wa zamani mulamwah. “Wakati maisha inakupa sababu mia moja ya kuangua kilio na kuhuzunika, una jukumu la kuonesha maisha sababu millioni moja ya kutabasamu na kushukuru. Baki na nguvu,” Ameandika Caroll Sonnie kupitia Instastory yake. Utakumbuka juzi kati Mulamwah aliibuka kupitia mitandao yake ya kijamii na kufunguka mengi kuhusu maisha yake ya ndani kwa kusema kwamba alivunja mahusiano yake na Carol Sonnie baada ya mrembo huyo kumsaliti kimapenzi kwa kutoka na mwanaume mwingine. Haikushia hapo alienda mbali zaidi na kumkana mtoto aliyezaa na Carol Sonnie kwa kusema kuwa sio wake kwa kusema mtoto huyo sio wake.

Read More
 BABY MAMA WA MULAMWAH, CAROL MUTHONI AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA MADINI CLASSIC

BABY MAMA WA MULAMWAH, CAROL MUTHONI AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA MADINI CLASSIC

Baby Mama wa mchekeshaji Mulamwah, Carol Muthoni amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ishu ya kutoka kimapenzi na msanii Madini Classic. Kupitia Instagram page yake Carol Muthoni amepuzilia mbali suala la kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii huyo huku akionesha kushangazwa na kitendo cha Madini Classic kutumia jina lake kutafuta kiki  ya kutangaza ujio wa wimbo wake mpya. Mrembo huyo amewataka mashabiki zake kutoamini madai yanaosambaa mtandaoni kuwa anatoka kimapenzi na Madini Classic kwa kusema kuwa walikuwa wanatayarisha video ya wimbo mpya ya msanii huyo. Kauli ya Carol Muthoni imekuja mara baada ya Madini Classic kushare picha ya pamoja na mrembo wakiwa kwenye pozi la kimahaba zaidi ambapo alienda mbali zaidi na kuthibitisha kuwa mrembo huyo amekubali kuwa mke wake wa pili

Read More
 BABY MAMA WA MULAMWAH CAROL SONNIE AWACHARUKIA WANAOMPONDA MTANDAONI

BABY MAMA WA MULAMWAH CAROL SONNIE AWACHARUKIA WANAOMPONDA MTANDAONI

Baby mama wa mchekeshaji Mulamwah, Carol Sonnie amesikitisha na namna baadhi ya watu ambao wameanza kufanya mzaha na ishu ya kuachana na mchekeshaji huyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Carol Sonnie ameandika waraka mrefu akiwataka wanaotumia picha yake wakidai kwamba wanachumbia kushusha picha hizo ujumbe ambao umetafsiriwa unamlenga mchekeshaji Propesa ambaye juzi kati alipost picha ya mrembo huyo akidaiwa kuwa ni wapenzi. Mrembo huyo ambaye ni mtoto wa mmoja amesema kitendo hicho sio cha kingwana ikizingatiwa kuwa inamharibia sifa mbele ya umma pamoja na mtoto wake. Hata hivyo amewatolea uvivu wale ambao wanashinikiza afanye vipimo vya DNA kubaina kama kweli mtoto wake huyo ni wa Mulamwah kwa kusema kwamba jambo hilo ni lake na Baby Daddy wake huku akisisitiza kuwa kuachana kwao haihusiani na mtoto wao. Ikumbukwe Mulamwah ambaye ni baba ya mtoto mmoja kwa sasa na baby mama wake Carol Sonnie waliweka wazi uhusiano wao mwaka wa 2017.

Read More