CAVANI BADO YUPO YUPO MANCHESTER UNITED
Baada ya tetesi kuwa staa wa Uruguay ambaye anaichezea Manchester United, Edson Cavani anasitisha mkataba wake na klabu hiyo ya England, majibu yamepatikana. Ralf Rangnick ambaye ni kocha wa timu hiyo amethibitisha kuwa Cavani bado yupo Manchester United na hana mpango wa kuhamia Barcelona kama ilivokuwa ikidaiwa. βCavani hatoondoka Januari hii, tulikaa nae tukaelewana vizuri na yeye anajua sitamuacha aende. “Cavani ni mchezaji mzuri, na nilimwambia tangu siku ya kwanza na ni mchezaji muhimu, haendi kokote bado tupo naye,β – Amesema Ralf Rangnick kwenye moja ya interview. Mkataba wa Cavani na Manchester United unatarajia kufika kikomo Juni mwaka huu 2022, na hapo mchezaji huyo ataamua kama ataendelea na timu hiyo ama ataachana nayo ila kwa sasa bado yupo yupo.
Read More