ChatGPT Kuanza Kuonyesha Matangazo kwa Watumiaji wa Bure

ChatGPT Kuanza Kuonyesha Matangazo kwa Watumiaji wa Bure

Kampuni ya OpenAI inajipanga kuanza kuweka matangazo kwa watumiaji wa bure wa ChatGPT, ikiwa ni sehemu ya mpango mpya wa kuongeza mapato. Taarifa zinaonyesha kuwa mfumo mpya wa apps za ChatGPT umeanza kuonyesha misimbo ya aina mbalimbali za matangazo, ikiwemo search ads, ad carousel na hata API maalum ya kuendesha matangazo hayo. Mpango huo unatarajiwa kuenea kwenye majukwaa ya iOS, Mac pamoja na toleo la tovuti. Hatua hii inaelezwa kuwa njia ya kuimarisha mapato, hasa kwa kuwa huduma za Plus zinazotozwa dola 20 kwa mwezi na Pro dola 200 kwa mwezi, hazina matangazo na zinategemea ada za wanachama. Aidha, kuna dalili za kupandishwa bei kwa baadhi ya huduma za kulipia. Kwa sasa, matangazo yanaripotiwa kuonekana zaidi katika kitengo cha search, na hasa pale watumiaji wanapouliza maswali yahusuyo bidhaa za kununua.

Read More
 Spotify Yashirikiana na ChatGPT Kuboresha Uzoefu wa Kusikiliza Muziki

Spotify Yashirikiana na ChatGPT Kuboresha Uzoefu wa Kusikiliza Muziki

Kampuni ya huduma ya muziki mtandaoni, Spotify, imeingia kwenye ushirikiano na ChatGPT kwa ajili ya kuboresha namna watumiaji wanavyogundua na kusikiliza muziki. Ushirikiano huu umezaa kipengele kipya kinachowezesha watumiaji kuwasiliana moja kwa moja na ChatGPT ili kutengeneza orodha za nyimbo, kupata mapendekezo, na kusikiliza muziki kupitia Spotify. Kupitia teknolojia hii, watumiaji wa Spotify wanaweza kuomba ChatGPT iwasaidie kutengeneza playlists kulingana na hisia au shughuli zao. Kwa mfano, mtu anaweza kuandika, “Nahitaji muziki wa kunituliza baada ya kazi,” na ChatGPT itapendekeza nyimbo zinazolingana na hali hiyo. ChatGPT pia inaweza kutumia historia ya kusikiliza ya mtumiaji kwenye Spotify ili kutoa mapendekezo yanayoendana na ladha yao ya muziki. Kwa kuelewa vizuri kile ambacho mtumiaji amekuwa akisikiliza, ChatGPT hutoa mapendekezo ya nyimbo au wasanii wapya kwa usahihi zaidi. Ushirikiano huu unaleta urahisi kwa watumiaji wanaotafuta njia za haraka, rahisi na za kibinafsi zaidi za kugundua muziki mpya. ChatGPT pia inaweza kusaidia kupendekeza nyimbo kwa misingi ya maelezo ya wazi kutoka kwa mtumiaji, bila ya kuwa na ujuzi maalum wa kutafuta muziki kwenye programu ya Spotify. Kipengele hiki tayari kinapatikana kwa baadhi ya watumiaji wa ChatGPT Plus, na kimepokelewa kwa shangwe na wengi wanaotafuta njia rahisi ya kufurahia muziki kwa njia ya mazungumzo ya moja kwa moja na akili bandia.

Read More