Cheed na Killy wafuta urafiki na Harmonize Instagram

Cheed na Killy wafuta urafiki na Harmonize Instagram

Wasanii Cheed na Killy huenda kwa sasa wakawa hawataki kuona chochote kuhusu Harmonize. Wawili hao wameamua kumu-unfollow bosi wao huyo wa zamani katika kurasa zao za Instagram baada ya lebo ya Konde Music Worldwide kusitisha mkataba wao kwa sababu ambazo hawakuziweka wazi. Utakumbuka mwisho mwa wiki iliyopita, Cheed na Killy waliwasilisha lalama zao kwa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kupata mwanga kuhusu sakata la kutimuliwa kwao. Lakini kikao cha kutatua mgogoro wao na lebo hiyo hakikuweza kufanyika baada ya uongozi wa Konde Music Worldwide kushindwa kufika Basata.

Read More
 Killy na Cheed waishtaki lebo ya Konde Music Worldwide kwa kuvunja mkataba wao

Killy na Cheed waishtaki lebo ya Konde Music Worldwide kwa kuvunja mkataba wao

Mambo yanazidi kuwa mengi baada ya wanamuziki Killy na Cheed kuondoshwa katika lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide ambapo wasanii hao wameripotiwa kufika Baraza la Sanaa Tanzania BASATA kwa madai ya kufuatilia na kukamilisha mchakato wa kuachana na lebo hiyo. Meneja wa wasanii hao Sats Sembe, amesema sababu ya wao kufikisha malalamiko yao Basata ni kupinga utaratibu wa kuvunja mkataba na wasanii hao ambapo ameeleza kuwa hakuna barua yoyote ya maandishi waliopewa mpaka sasa. Sembe amesema kwa kuwa waliingia lebo ya Konde kwa maandishi basi hata kuondoka wanapaswa kuondoka kwa maandishi, ili kesho isije kutokea sintofahamu katika masuala ya kisheria. “Huko mbeleni hatujui hili suala litafika hapa, lakini kwa kuanzia tumeanzia kwa walezi wetu na wazazi wetu Basata ambao katika hali ya kawaida tusingeweza kuwaruka. “Lakini kama ikishindikana hatua hii tutaeda hata mahakamani ambapo kote huku barua ya maandishi ni muhimu kama ushahidi kwamba wameachana na wasanii”

Read More
 Cheed na Killy waondoka rasmi Konde Gang

Cheed na Killy waondoka rasmi Konde Gang

Lebo ya Konde Music Worldwide inayomilikiwa na Harmonize imetangaza rasmi kusitisha mkataba na wasanii wake wawili Cheed na Killy kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao. Lebo hiyo ambayo leo imetimiza miaka 4 tangu kuanzishwa kwake Oktoba 10, mwaka 2019, iliwasajili Cheed na Killy Septemba mwakaa 2020 wakitokea lebo ya King’s Music ya Ali Kiba Wasanii hao wanaungana na rapa Country Boy ambaye alijitoa Konde Music mapema mwa mwaka huu. Kwa miaka miwili waliyokuwepo Konde Music,Killy aliweza kutoa Greenlight EP yenye jumla ya nyimbo 5 huku Cheed akiachia Endless love EP yenye jumla ya ngoma 6 za moto.

Read More
 CHEED ADOKEZA UJIO WA EP YAKE MPYA

CHEED ADOKEZA UJIO WA EP YAKE MPYA

Staa wa muziki kutoka Konde Gang Cheed ametangaza kuachia EP yake ya kwanza tangu ajiunge na lebo hiyo ya muziki inayomilikiwa na Harmonize. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Cheed ameachia swali kwa mashabiki zake kama wapo tayari kuipokea EP yake mpya inayosomokea  “Are you ready for my first Extended Playlist?! Stay ready!! 🚨#Cheed #Kondegang4you” Pamoja na kutoa taarifa hiyo, Cheed hajaweka wazi jina la EP hiyo pamoja na tarehe ya kuachia EP yenyewe. Cheed atakuwa msanii wa pili kuachia ndani ya mwaka huu baada ya Killy ambaye aliwabariki mashabiki zake za Green light EP yenye jumla ya nyimbo 5 za moto.

Read More