“Warembo Wanapenda Mali, Sio Ndoa” – Msanii Chris Evans

“Warembo Wanapenda Mali, Sio Ndoa” – Msanii Chris Evans

Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Chris Evans, ametangaza rasmi kuachana na wanawake warembo, akisema hawana nia ya dhati ya kuingia kwenye ndoa. Evans, ambaye amewahi kuhusishwa kimapenzi na mastaa kama Zanie Brown, Spice Diana, na Lydia Jazmine, amesema kwamba wanawake wengi warembo huwa wanavutiwa na mali na si kujenga familia. Mwanamuziki huyo anayefahamika kwa kibao chake maarufu “Linda”, amesema kwa sasa moyo wake umeelekezwa kwa wanawake wa muonekano wa wastani, ambao kwa mtazamo wake wana sifa ya unyenyekevu, uaminifu, na nia ya kweli ya kuanzisha ndoa ya kudumu. “Nimeacha kuwahangaikia wanawake warembo kwa sababu hawana nia ya kweli. Wengi wao wanawinda pesa na hata hawafai kwa ndoa. Nitawachagua wale walio na mwonekano wa wastani kwa sababu huwa ni uaminifu na wako tayari kuanzisha maisha ya ndoa,” alieleza. Chris Evans amesisitiza kuwa yuko tayari kutulia na mwanamke mmoja na kuanzisha familia yenye misingi imara ya upendo na uaminifu Hatua hii inaonekana kuwa mwanzo mpya kwa msanii huyo mkongwe, ambaye kwa muda mrefu ameonekana kwenye vichwa vya habari kutokana na mahusiano yake ya kimapenzi na mastaa wa tasnia ya burudani nchini Uganda.

Read More
 CHRIS EVANS AKANUSHA MADAI YA KUFUNGA NDOA NA MARY BATA

CHRIS EVANS AKANUSHA MADAI YA KUFUNGA NDOA NA MARY BATA

Mwanamuziki wa bendi kutoka Uganda Chris Evans amepuzilia mbali madai kuwa ana mpango wa kutambulishwa nyumbani kwa msaniii mwenzake Mary Bata kama mume mtarajiwa wa msanii huyo kwa njia ya harusi ya kitamaduni. Chris evans amesema ameshangazwa  kuona barua ya mwaaliko ya harusi inayosambaa mtandaoni huku  akisema kuwa barua hiyo ni batili kwani hana mpango wa kumtambulisha msanii huyo kwa wazazi wake. Chris Evans amesema Mary Bata ni rafiki yake na ikitokea amemtambulisha kwa wazazi wake hawezi kataa ila kwa sasa hawana uhusiano wowote wa kimapenzi na mwanamama huyo. “I didn’t know about this occasion. Mary Bata is my friend, if she chooses to introduce me, then I won’t refuse, but we don’t have such plans. I am not romantically involved with her. I don’t want to be embarrassed,” amesema Chris Evans. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wanahoji kuwa wawili hao walipanga tukio hilo kama njia ya kutangaza wimbo wao mpya uitwao Tubaale.

Read More
 CHRIS EVANS AWATAKA WALIMENGU WAMPE UHURU WA KUIKUZA PENZI LAKE NA MREMBO BRISHER KASH

CHRIS EVANS AWATAKA WALIMENGU WAMPE UHURU WA KUIKUZA PENZI LAKE NA MREMBO BRISHER KASH

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Chris Evans ametoa rai kwa mashabiki zake pamoja na vyombo vya habari kutoingilia mahusiano yake na malkia wa tiktok nchini humo Brisher Kash wakati huu penzi lao linazidi kukolea. Katika mahojiano yake hivi karibuni Chris Evans amedai kuwa kadri watu wanavyozidi kumfuatilia na kumuuliza maswali kuhusu maisha yake ya mahusiano, ndivyo wanatengeneza mazingira ya mrembo huyo kumkimbia kwani huenda akatamka maneno yanayokinzana na yale aliyomuambia kipindi wanaanza kuchumbiana. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Linda” amewataka walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wampe uhuru wa kuikuza penzi lake na Brisher Kash bila muingilio wowote. Chris Evans na Brisher Kash wamekuwa wakionekana kwenye viwanja mbali mbali vya kukulia bata viunga mwa jiji la Kampala kwa wiki kadhaa sasa jambo ambalo limewaaminisha watu wengi kuwa huenda wawili hao wanatoka kimapenzi.

Read More