CHRIS ROCK: SITAONGELEA SAKATA LA WILL SMITH  KUNIPIGA KOFI HADI NILIPWE

CHRIS ROCK: SITAONGELEA SAKATA LA WILL SMITH KUNIPIGA KOFI HADI NILIPWE

Mchekeshaji kutoka Marekani Chris Rock amesema hatozungumzia sakata la kuchapwa kofi na Will Smith hadi pale atakapolipwa pesa. Mchekeshaji huyo alizungumza hayo mbele ya wahudhuriaji wa onesho lake juzi Ijumaa, ambapo alisema “Mimi niko sawa, nina hii show nzima, lakini sitaongelea kuhusu hilo hadi pale ambapo nitalipwa. Maisha ni mazuri, nimerudisha hali yangu ya kusikia.” Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, wameichambua kauli hiyo na kusema kwamba pengine Chris Rock anataka kulipwa pesa ndefu kwa ajili ya kufanya mahojiano maalum kuhusu tukio lile. Au pia ana mpango wa kufungua kesi dhidi ya Will Smith ambapo atalipwa pesa ndefu.

Read More
 BEI YA TIKETI ZA TAMASHA LA CHRIS ROCK YAONGEZEKA MARADUFU HUKU ZIKINUNULIWA KWA WINGI

BEI YA TIKETI ZA TAMASHA LA CHRIS ROCK YAONGEZEKA MARADUFU HUKU ZIKINUNULIWA KWA WINGI

Mchekeshaji Chris Rock ameripotiwa kuvuna pakubwa kutokana na umaarufu wa muda alioupata baada ya kupigwa kofi na mwigizaji na mwanamuziki Will Smith. Tukio hilo lililojiri Machi 27, 2022 katika ukumbi wa maonyesho wa Dolby huko Los Angeles. Rock alikuwa jukwaani kwa ajili ya kukabidhi tuzo ya Oscar, kilichosababisha apigwe kofi ni baada ya kutania hali ya mke wa Will Smith ya kupoteza nywele kichwani. Rock alikuwa amepanga onyesho la vichekesho katika sehemu mbalimbali ambalo amelipa jina la “Ego Death Comedy Tour” ambalo litaanza rasmi Aprili 2 huko New Jersey nchini Marekani na ripoti mbalimbali zinaeleza kwamba viti vyote tayari vimelipiwa. Kabla ya ziara hiyo ya mchekeshaji Chris Rock, amepanga onyesho katika ukumbi wa Wilbur huko Boston na tiketi za onyesho hilo ziliongezwa bei na kuuzwa kwa wingi zaidi. Kampuni moja maarufu ya uuzaji tiketi za maonyesho iitwayo “TickPick” iliandika kwenye Twitter kwamba wameuza tiketi nyingi zaidi za wanaotaka kumuona Chris Rock akichekesha kwa usiku mmoja ikilinganishwa na jumla ya tiketi ambazo waliuza kwa maonyesho yake ya mwezi mmoja uliopita. TickPickiumeripoti kwamba mauzo ya tiketi kwa ziara hiyo ya ucheshi yamepanda mara 200, wanasema machi 28 tiketi zilinunulika zaidi baada ya tukio la chris rock kupigwa kofi huku bei zikipanda kutoka shilling elfu 5, kwa tiketi hadi elfu 39 za Kenya.

Read More