Perplexity Yajitokeza kwa Ofa Kubwa ya Kununua Chrome
Kampuni ya Perplexity, inayojulikana kwa app yake inayoshindana na ChatGPT, Grok, na DeepSeek, imeweka ofa ya Dola Bilioni 34.5 kununua browser maarufu ya Chrome. Google inahofia kuuza browser hii kwani inatumia Chrome kujiwekea faida, kuweka matangazo, na kukusanya data nyingi za watumiaji duniani. Hadi sasa, Google haijaonyesha muamko rasmi, na ina mpango wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya Marekani unaolenga kupunguza nguvu zake. Chrome ni browser inayotumika zaidi duniani ikilinganishwa na Safari na Firefox, na ni kitovu cha mawasiliano, matangazo, na matumizi ya AI. Perplexity inaamini kumiliki Chrome kutawapa mamilioni ya watumiaji, kuwapa nafasi ya kueneza huduma zao za AI na kuleta ushindani dhidi ya kampuni kubwa kama OpenAI. Ingawa thamani ya Perplexity ni Bilioni 20, kampuni hiyo imeonyesha nia kubwa kwa kutoa ofa ya Bilioni 34.5 kununua Chrome. Hii inaweza kuwa hatua kubwa ya kuipita ChatGPT kwa watumiaji wengi zaidi. Hali hii inaonyesha kampuni za AI zinafanya mikakati ya kununua browsers, huku OpenAI pia ikiandaa kuwa na browser yake binafsi.
Read More