CIARA AKAVA JARIDA LA EBONY, AFUNGUKA KUHUSU ALBUM YAKE MPYA

CIARA AKAVA JARIDA LA EBONY, AFUNGUKA KUHUSU ALBUM YAKE MPYA

Mwimbaji nyota wa RnB kutoka Marekani Ciara amelibariki jarida la Ebony toleo la mwezi, Septemba ambapo amefunguka mambo kibao kuhusu muziki, maisha na mengine mengi. Kubwa zaidi ambalo mrembo huyo amelizungumzia ni kuhusu ujio wa album yake mpya ikiwa ni baada ya miaka 3 alipoachia, Beauty Marks. Ciara amesema mategemeo yake ni dunia nzima icheze kwa sababu ngoma zilizopo kwenye Album hiyo zina ‘energy’ ya kutosha. Tayari ametanguliza wimbo wa kwanza kutoka kwenye album hiyo “Jump” ambao ulitoka mwezi Julai mwaka huu.  

Read More
 CIARA MBIONI KUACHIA ALBUM MPYA

CIARA MBIONI KUACHIA ALBUM MPYA

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Ciara ametangaza kurejea kwenye muziki baada ya ukimya wa miaka mitatu. Hitmaker huyo wa ngoma ya ‘Level Up” amedokeza ujio wa Album yake mpya ambayo itakuwa ya Nane tangu aanze safari yake ya muziki mwaka 2002. Kwa mujibu wa taarifa, inaelezwa kuwa tayari amekamilisha video ya wimbo wake wa kwanza uitwao “Jump” ambao utapatikana kwenye Album hiyo. Mara ya mwisho Ciara kutubariki na Album ilikuwa Mwaka 2019 alipoachia Album iitwayo “Beauty Marks ambayo ilikuwa na jumla ya mikwaju 10 ya moto.

Read More