CLEVER J AFUNGUKA KUNYANYASWA NA PALLASO PAMOJA NA CHAMELEONE

CLEVER J AFUNGUKA KUNYANYASWA NA PALLASO PAMOJA NA CHAMELEONE

Msanii mkongwe kwenye muziki kutoka nchini Uganda Clever J ameonekana kukerwa na hatua ya Pallaso pamoja na Chameleone kushindwa kumlipa pesa zake licha ya kutumbuiza kwenye shows zao. Katika mahojiano yake hivi karibuni CleverJ ameamua kutoa ya moyoni kwa kusema kwamba licha kutokea kwenye shoo sita za wawili hao hajapokea malipo yeyote. kwao. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Manzi Wanani” ametoa changamoto kwa Chameleone pamoja na mdogo wake Pallaso wamlipe haki yake akisema itakuwa ni jambo la aibu kwake kuanza kuwa omba omba ikizingatiwa kuwa watu wamekuwa wakimuona akitumbuiza kwenye shows mbali mbali. Licha ya Clever J kuibua madai hayo Pallaso na Chameleone hawajatoa tamko lolote kuhusu tuhuma zilizoibuliwa na msanii huyo ila ni jambo la kusubiriwa.

Read More
 CLEVER J: KIBURI IMENIPONZA KISANAA

CLEVER J: KIBURI IMENIPONZA KISANAA

Msanii mkongwe kwenye muziki kutoka nchini Uganda Clever J amekiri kuwa kitendo chake cha kutokubali kusimamiwa kikazi ndio imemponza kisanaa kwa miaka mingi. Katika mahojiano yake ya hivi karibu hitmaker huyo wa ngoma ya “Manzi wa Nani” amesema hawezi stawi katika mazingira ya kupewa masharti ikizingatiwa kwamba hapendi kuwa chini ya shinikizo. “Niliwaambia nyie kwamba mimi ni mtu mgumu sana. Sasa nataka kufanya mambo nipendavyo bila kuomba ruhusa,” alisema Clever Utakumbuka Clever J alipata uongozi mpya miaka kadhaa iliyopita kwa ajili ya kuufuafua muziki wake lakini mwanamuziki huyo aligura uongozi wake huo na kuanza kufanya shughuli zake kama msanii wa kujitegemea. Clever J alipata umaarufu kwenye muziki Afrika Mashariki mwaka wa 2007 kupitia wimbo wake uitwao “Manzi wa Nani” na alianza shughuli zake za kimuziki katika lebo ya muziki ya Leone Island inayomilikiwa na Jose Chameleone kabla ya kuondoka na kuhamua kuwa msanii wa kujitegemea.

Read More