Rapa Country Wizzy mbioni kuja na Yule Boy Album sehemu ya pili

Rapa Country Wizzy mbioni kuja na Yule Boy Album sehemu ya pili

Rapa kutoka nchini Tanzania Country Wizzy ameweka wazi kuja na sehemu ya pili ya album yake ya Yule Boy ambapo sehemu ya kwanza ya album hiyo ilitoka mwaka 2019 ikiwa na jumla ya ngoma 30. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, ametangaza kuwa ni muda wa studio sasa kwa ajili ya kuandaa sehemu ya pili ya album ya Yule Boy. “Studio time for Yule Boy Album Part 2…, see yall when the music is ready”, Aliandika. Itakumbukwa, sehemu ya kwanza ya album ya Yule Boy iliwakutanisha wakali wengine kama Moni Centrozone, Harmonize, Mwana FA, Khaligraph Jones, G Nako, na Mimi Mars.

Read More
 COUNTRY WIZZY MBIONI KUJA NA BRAND YAKE YA MAVAZI

COUNTRY WIZZY MBIONI KUJA NA BRAND YAKE YA MAVAZI

Rappa kutoka Tanzania Country Wizzy ameweka wazi mpango wake wa kuingia kwenye baishara ya mavazi ambapo amesema kabla ya mwaka huu kuisha atakuwa tayari ameshafungua duka lake la nguo. Mkali huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake “You” ametambua kuwa kwa hatua aliyofikia, si muziki wake pekee unaouza, bali ni jina lake ndilo lenye thamani zaidi ya kitu chochote kwa sasa. Kwa mtaji wa jina lake na wafuasi wake, anaweza kutengeneza fedha nyingi zaidi kupitia biashara. Kwenye posti yake aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Country Wizzy pia amewataka mashabiki wake wampe jina la duka hilo huku komenti zikiwa nyingi na zote zikipendekeza duka lake kuitwa Country Boy.

Read More
 COUNTRY WIZZY ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA

COUNTRY WIZZY ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA

Rappa kutoka Tanzania Country Wizzy ametudokeza juu ya ujio wa sehemu ya pili ya Album yake Yule Boy Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa instagram amesema album yake ya “Yule Boy Part 2” itaingia sokoni ndani ya mwaka huu. Country ambaye kwa sasa anamiliki lebo yake ya muziki, “Yule Boy” ni album yake ya kwanza tangu aanze muziki wake, na ilitoka Novemba mwaka 2019, ikiwa na jumla ya nyimbo 31. Country Wizzy anafanya poa ngoma yake iitwayo Shauri Lako ambayo ndani kipindi cha mwezi mmoja imefikisha Zaidi ya views laki 3 youtube.

Read More
 RAPPER COUNTRY BOY AMALIZA MKATABA WAKE NA KONDE MUSIC WORLDWIDE

RAPPER COUNTRY BOY AMALIZA MKATABA WAKE NA KONDE MUSIC WORLDWIDE

Msanii wa Bongofleva Country Boy ameachana rasmi na label ya Konde Music Worldwide kufuatia taarifa kwamba mkataba wake umemalizika. Kupitia page rasmi ya KondeGang katika mtandao wa Instagram ,imethibitisha taarifa hiyo kwa kuandika ujumbe wa kumuaga na kumtakia maisha mapya, huku wakiweka wazi kuwa mkataba wake umemalizika rasmi tarehe 8 Januari mwaka wa 2022 kwa makubaliano ya pande zote mbili. Mpaka sasa rapper huyo hajazungumza chochote kuhusu taarifa hiyo, huku kukiwa na minong’ono mingi kuhusu sababu iliyo-elekea rapper huyo kutemana na record label hiyo iliyo chini ya mwanamuziki Harmonize huku hali ikitajwa kutokua shwari kwa wasanii wengine. Country Boy (Country Wizzy) alisainiwa Konde Music Worldwide September 11, mwaka wa 2020 na kuachia kazi kadha ikiwemo EP yake “The Father EP” pia hits kibao kama Baby, Say, BABA na nyingine.

Read More