Vincent Aboubakar avunjiwa mkataba Al Nassrna kisa Ronaldo
Klabu ya Al Nassr imevunja mkataba na mshambuliaji Vincent Aboubakar kwa makubaliano ya pande zote mbili ili kutoa nafasi moja ya mchezaji wa kigeni kwa ajili ya kumsajili Cristiano Ronaldo. Mamlaka ya soka ya Saudi Arabia inatuhusu wachezaji 8 tu wa kigeni lakini kwa sasa klabu hiyo ina jumla ya wachezaji 9 pamoja na Ronaldo hivyo Aboubakar amelazimika kufanyika kondoo wa kuteketezwa (sacrificial lamb). Kwa mujibu wa ripoti mshambuliaji huyo raia wa Cameroon amepokea ofa nzuri Barani Ulaya huku Manchester United ikiwa moja ya vilabu vinavyomlenga.
Read More