DaBaby Ashinda Kesi ya Shambulio Dhidi ya Kaka wa DaniLeigh Lakini Bado Yuko Hatiani Kifedha

DaBaby Ashinda Kesi ya Shambulio Dhidi ya Kaka wa DaniLeigh Lakini Bado Yuko Hatiani Kifedha

Msanii maarufu wa hip hop, DaBaby, amepata ushindi wa kisheria baada ya jaji mmoja wa Los Angeles kutupilia mbali madai ya kushambulia yaliyowasilishwa na Brandon Bills, ndugu wa aliyekuwa mpenzi wake, DaniLeigh, kuhusu ugomvi uliotokea kwenye uwanja wa bowling mwaka 2022. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Billboard Hip Hop, jaji alitupilia mbali kesi hiyo kwa sababu ya kushindwa kumkabidhi DaBaby hati za madai ndani ya muda uliowekwa kisheria. Licha ya ushindi huo, DaBaby bado anakabiliwa na madai ya kifedha yanayotokana na uharibifu wa mali katika uwanja huo wa bowling, ambapo waendeshaji wa sehemu hiyo wanadai fidia kupitia dai la kisheria la “indemnity” (fidia kwa uharibifu uliofanywa na mteja wake). Kesi hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa rasmi mnamo msimu wa vuli wa mwaka 2026. Ugomvi huo wa hadharani ulichukua nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari mwaka 2022, baada ya video za DaBaby na Brandon Bills wakizozana na kupigana hadharani kusambaa mitandaoni. Tukio hilo lilizua hisia kali kutoka kwa mashabiki na wanaharakati wa haki za kijamii. Kwa sasa, ingawa amejinasua kwenye madai ya moja kwa moja ya kushambulia, DaBaby anasalia na safari ya kisheria mbele yake kuhusu athari za tukio hilo kwa biashara ya uwanja wa bowling.

Read More
 MEGAN THEE STALLION AJIBU TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA DABABY

MEGAN THEE STALLION AJIBU TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA DABABY

Rapa kutoka Marekani Megan Thee Stallion ni kama amemjibu DaBaby baada ya kufunguka kwenye ngoma yake mpya kwamba alifanya mapenzi na Megan siku moja kabla ya tukio ambalo anadai kupigwa risasi mguuni na Tory Lanez. DaBaby alifunguka hayo kupitia ngoma yake mpya “BOOGYMAN” na kusema amekuwa akitoka na Megan mara kibao tu. Sasa ni kama Thee Stallion ameamua kumjibu DaBaby ambapo akiwa Jukwaani kwenye Tamasha la iHeartRadio, alisikika akisema “Sifahamu kuhusu ninyi, lakini Mimi binafsi naupenda sana mwili wangu.” ishara ya kukanusha yote yaliyoimbwa na DaBaby.

Read More
 DAVIDO NA DABABY WAONEKANA LAGOS KUKAMILISHA COLABO YAO

DAVIDO NA DABABY WAONEKANA LAGOS KUKAMILISHA COLABO YAO

Rapa kutoka Marekani, Dababy ameonekana Nigeria akiwa pamoja na Davido ambaye ndiye kama mwenyeji wake nchini humo. Wawili hao walionekana wakizunguka katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Lagos, huku kila mmoja akishare baadae video wakiwa pamoja kupitia mitandao yao ya kijamii. Aidha, Dababy ametumia ukurasa wake wa Instagram kumshukuru Davido kwa kumfanya ajisikie yupo nyumbani. “Davido amenifanya nijisikie kama nipo nyumbani ”, Ameandika Dababy. Utakumbuka Dababy ametua nchini Nigeria akitokea Ujerumani, ambapo yupo nchini humo kwa ajili ya kukamilisha video ya collabo yake na Davido.

Read More
 DABABY AKANUSHA UVUMI WA KUMNG’OA MTU JINO KWA NGUMI

DABABY AKANUSHA UVUMI WA KUMNG’OA MTU JINO KWA NGUMI

Rapa kutoka Marekani DaBaby ambaye yupo midomoni mwa watu baada ya kuenea kwa taarifa zake kuwa alishtakiwa kwa kosa la jinai baada ya Gary Prager, meneja wa mali, kumshutumu yeye na timu yake kwa kumshambulia na kumng’oa jino mwaka wa 2020. Kufuatia kuenea kwa kasi kwa taarifa hizo hatimaye rappa DaBaby amejibu kwa mara ya kwanza kuhusu madai hayo. Kupitia video aliyopost kwenye ukurasa wake wa instagram, DaBaby ameonekana kukarisirishwa na kitendo cha kusambazwa kwa taarifa hizo ambazo amedai kuwa ni za uongo licha ya kufikishwa kwenye mamlaka za usalama nchini humo. Utakummbuka Mwaka wa 2020 iliripotiwa kwamba dababy alikodisha nyumba kwa ajili ya kufanya video, na walikubaliana na mwenye nyumba kuingiza watu 12 tu ndani kulingana na kanuni za COVID-19. Kinyume na masharti, DaBaby aliingiza watu takribani 40, mwenye nyumba hiyo Gary Pagar alipoamua kumfuata kwa kuvunja masharti ya mkataba, mtu mmoja kutoka kambi ya DaBaby alimvamia na kumuangusha chini. Baada ya hapo DaBaby alitoka kwenye gari na kumkimbiza pagar hadi ndani nyumba ambapo alianza kwa kumuonya kutowapa taarifa polisi kisha alimtwanga mangumi ya uso hadi kumng’oa jino.

Read More
 DABABY KUFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUMPIGA NGUMI NA KUMG’OA MTU JINO

DABABY KUFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUMPIGA NGUMI NA KUMG’OA MTU JINO

Rapa kutoka Marekani DaBaby anakabiliwa na mashtaka ya jinai kwa kuhusishwa na kesi ya kumpiga mwanamume mmoja anayedaiwa kujaribu kuwazuia wasaidizi wa rapa huyo kufanya video ya muziki katika eneo lake Rapa huyo amefunguliwa mashtaka ya uhalifu na ofisi ya mwanasheria wa wilaya huko Los Angeles kufuatia tukio lililotokea mapema mwezi Desemba mwaka jana 2021 ambalo linadaiwa kumsababishia majeraha mabaya Gary Pagar ambaye ni mmiliki wa jumba hilo walilopangisha. Pagar aliwasilisha kesi kwa vyombo vya usalama mapema Februari, akidai alishambuliwa kwa kutekeleza sheria za msingi za kukodisha nyumba yake ambayo rapa Dababy alikodishiwa kwa ajili ya mapumziko mafupi ya likizo. Miongonia mwa masharti aliyotoa baba mwenye nyumba huyo ni kuwa DaBaby hakuruhusiwa kuwa na wageni zaidi ya 12 kwa wakati mmoja ndani ya jengo hilo la kifahari Baada ya kipindi cha wiki mbili Pagar anasema alibaini kwamba kulikuwa na zaidi ya watu 12, jambo lililompelekea kuilalamikia timu ya DaBaby kwa kukiuka makubaliano yao ya awali. Ilipofika Desemba 2, anasema alitembelea nyumba hiyo yeye mwenyewe na kugundua kwamba walikuwa wakirekodi video ya muziki na kikundi kizima cha filamu na idadi kubwa ya watu ambao anakadiria kuwa walifika zaidi ya 40, jambo lililomfanya ajaribu kuwazuia kuendelea na shughuli hiyo kwa kuwa tayari wamevunja utaratibu. Na hapo ndipo anapodai kuwa alianza kushambuliwa na mmoja wa wafanyakazi wa rapa DaBaby, sehemu ambayo kwa bahati ilinaswa kwenye video,Pagar anadai kuwa baada ya muda mfupi DaBaby alimuamuru mfanyakazi wake huyo kuacha kumshambulia lakini aliendelea kumpiga ngumi usoni hadi kumsababishia jino lake kung’oka.

Read More