Daddy Andre afunguka madai ya kuharibu wimbo wa Fred Sebata
Msanii kutoka nchini Uganda Daddy Andre amewajibu wanaodai kuwa aliharibu wimbo wa msanii mkongwe Lord Fred Sebatanoting uitwao Sam Wange. Kwenye mahojiano yake karibuni amesema alijaribu kuupa wimbo huo ladha ya kisasa kwa kutumia mdundo tofauti ila mashairi yake yalisalia yalivyo kwa kuwa wimbo wenyewe una hakimiliki. Msanii huyo ameongeza kuwa kama mwenye wimbo angelalamika na toleo lao basi angewashtaki kwa kuharibu wimbo huo uliofanya vizuri kipindi cha nyuma. Mwezi uliopita Daddy Andre na Sheebah Karungi walipata ukosoaji mkubwa mtandaoni kwa kuurudia wimbo wa Sam Wange wake Fred Sebata,hatua ambayo ilichukuliwa kama kuwakosea wasanii wakongwe. Mashabiki walimshauri Daddy Andre kuwaheshimu wakongwe badala ya kufanya nyimbo zao bila kuzingatia ubora.
Read More