Albamu mpya Darassa kuingia sokoni Februari 7, 2025
Mwanamuziki wa Bongofleva Darassa amethibitisha ujio wa albamu yake mpya Take Away The Pain, ambayo inatarajiwa kuingia sokoni rasmi Februari 7, mwaka 2025. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Darassa ameielezea albamu hiyo kama tiba mbadala ya kiburudani huku akisisitiza kuwa ni kazi bora iliyoundwa kwa ajili ya mashabiki wake. “Hii ni tiba mbadala ya kiburudani. hii ni albam ya karne. This is recreation alternative therapy. this is the album of the century”, Aliandika Instagram. Mkali huyo wa ngoma ya “I like It” ameishukuru timu yake na wasanii wote walioshiriki kwenye albamu hiyo. “Asante sana my brothers and sisters kwa kushirikiana na sisi, kwa pamoja tumetengeneza kitu bora sana kwa watu wetu. Mmetupa nguvu, moyo, muda pamoja na ujuzi wenu, tunafahamu ni kitu cha thamani sana kwa mtu kutoa.” Aliandika Instagram. Albamu hiyo ina jumla ya nyimbo 15, ikihusisha kolabo na wasanii wakubwa kama Ali kiba, Harmonize, Mbosso, Zuchu, Bien, Jay Melody, Jovial, na wengine wengi.
Read More