DAVID LUTALO AKERWA NA UKABILA ILIOKITHIRI UGANDA

DAVID LUTALO AKERWA NA UKABILA ILIOKITHIRI UGANDA

Msanii kutoka Uganda David Lutalo ameonekana kukerwa na tatizo la ukabila linaloendelea miongoni mwa wananchi nchini humo. Kwenye tamasha lake la muziki lililomalizika wikiendi hii iliyopita Lutalo alilazimika kukatisha kwa muda kuwapa mashabiki burudani akiwa jukwaani na kuamua kuwapa somo waganda kuacha tabia ya kuwabaguana kwa misingi ya kikabila kwani hatua hiyo inarudisha nyuma nchini kimaendeleo. Haikushia hapo alienda mbali zaidi na kuwapongeza wasanii wa uganda kuendelea kusaidiana kwenye shughuli za muziki huku akisisitiza kuwa hiyo ndio njia pekee ya kukuza na kuupeleka muziki wao kimataifa. Mwishoni mwa juma lililopita David Lutalo aliandaa tamasha lake la muziki liitwalo “Kabisi Kadagala” tamasha ambalo lilipata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki na viongozi wakuu serikalini.

Read More
 DAVID LUTALO AWAJIBU WANAOMKOSOA KING SAHA KUWA KIONGOZI WA WASANII UGANDA

DAVID LUTALO AWAJIBU WANAOMKOSOA KING SAHA KUWA KIONGOZI WA WASANII UGANDA

Mwanamuziki David Lutalo amejiunga na orodha ya waimbaji wanaomuunga mkono King Saha kutua wadhfa wa urais wa Chama cha Wanamuziki wa Uganda (UMA). Katika mahojiano yake ya hivi karibuni David Lutalo amesema kwa miaka ambayo amemfahamu King Saha, alikuja akagundua kuwa msanii huyo ni mtu mwerevu tofauti namna watu wanavyochukulia. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mboona” amepuuzilia mbali madai ya watu wanaodai kuwa King Saha hawezi waongoza wasanii nchini Uganda kutokana na kuathirika na matumizi ya mihadarati. “Nasikia watu wakisema kwamba anavuta bangi, lakini nadhani gugu lake haliendi kichwani. Ni mtu mwenye mawazo mazuri unapotangamana naye,” Lutalo alisema. Lakini pia ameongeza kuwa King Saha ni mweelewa na anaweza fanya kazi vizuri na hata watu walio chini yake. Hata hivyo alitaka kuwania wadhfa wa urais wa muungano wa wanamuziki nchini uganda lakini alikuja akajiondoa katika kinyanganyiro hicho kutokana na kukosa vigezo stahiki. Utakumbuka David Lutalo anajulikana kuwa mtu asiyeweza kufikiwa kwa urahisi tangu umaarufu ulipomuingia kichwani mwake

Read More
 DAVID LUTALO AIPIGA CHINI SHOW YAKE YA PASAKA KISA BEBE COOL NA JOSE CHAMELEONE

DAVID LUTALO AIPIGA CHINI SHOW YAKE YA PASAKA KISA BEBE COOL NA JOSE CHAMELEONE

 Nyota wa muziki nchini Uganda David Lutalo amegonga vichwa vya habari nchini humo mara baada ya kufuta performance yake ya Siku Kuu ya Pasaka huko Freedom City.. Kupitia mitandao yake ya kijamii David Lutalo ameandika ujumbe wa kuwaomba radhi mashaiki zake kwa hatua ya kujiondoa kwenye tamasha hilo kutokana na mambo ambayo yapo nje ya uwezo wake. Hitmaker huyo wa ngoma ya “In Love” amewashukuru mashabiki kwa ushirikiano na upendo wao huku akiwataka waendelee kumfuatilia kwani ataanika mkeka wa shows zake hivi karibuni. Hata hivyo David Lutalo hajaweka wazi kilichompelekea kuchukua maamuzi ya kujiondoa kwenye tamasha hilo la siku ya pasaka ila wajuzi wa mambo wanadai kwamba waandaji wa tamasha hilo wameshindwa kuafikia vigezo vya msanii huyo kutumbuiza kwenye show hiyo upande wa malipo. Ikumbukwe David Lutalo alitarajiwa kushare steji moja na wasanii kama Bebe Cool pamoja na Jose Chameleone.

Read More