David Wonder aachia rasmi Album yake mpya

David Wonder aachia rasmi Album yake mpya

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya David Wonder ameachia rasmi Album yake mpya iitwayo “Mwanzo” Album hiyo ina jumla ya nyimbo 12 ambapo ni wanamuziki 4 pekee ndio waliopata shavu la kushirikishwa ndani ya album hiyo ambao ni Guardian Angel, Jabidii, Moji ShortBabaa na Hakuna Matata. Miongoni mwa watayarishaji waliohusu kuipika Album hiyo ni pamoja na Shallz baro, Sean on the Beat na Alexis on the Beat. Mwanzo ambayo ni Album ya kwanza katika safari ya muziki ya David Wonder  tayari inapatikana kupitia digital platforms zote za kupakua na kusikiliza muziki duniani.

Read More
 David Wonder atangaza rasmi tarehe ya kuachia album yake mpya

David Wonder atangaza rasmi tarehe ya kuachia album yake mpya

Mwanamuziki wa nyimbo za injiili Nchini David Wonder ametusanua kuwa album yake mpya iitwayo mwanzo imekamilika. Wonder amesema album yake itaingia sokoni rasmi Desemba 10 mwaka huu huku akiwa amewashirikisha wasanii mbali mbali wa nyimbo za injili kutoka Afrika Mashariki. Licha ya kutoweka wazi idadi ya nyimbo inayopatikana kwenye mwanzo album, David Wonder amewataka mashabiki wakae mkao wa kula kuipokea Album yake hiyo. Hii itakuwa ni album ya kwanza kwa mtu David Wonder tangu aanze safari yake muziki.

Read More
 DAVID WONDER ANYOSHA MAELEZO KUHUSU BIFU LAKE NA BAHATI

DAVID WONDER ANYOSHA MAELEZO KUHUSU BIFU LAKE NA BAHATI

Msanii wa nyimbo za injili nchini David Wonder amefunguka kuhusu ishu ya kuwa kwenye bifu na staa wa muziki nchini Bahati mara baada ya nyimbo zake alizofanya na msanii huyo akiwa chini ya lebo ya EMB kufutwa kwenye mtandao wa Youtube. Akipiga stori na mwanahabari Nicholas Kioko kwenye mtandao wa Youtube David Wonder amesema hana ugomvi wowote na msanii huyo licha ya kwamba amekuwa akimzungumzia vibaya kwenye mahojiano mbali mbali. Hitmaker huyo wa “Naenda na Yesu” amekanusha ishu ya kupotea kimuziki kwa kusema kwamba amekuwa akiachia ngoma bila kupoa ila vyombo vya habari nchini Kenya vimekuwa vikiwangazia wasanii ambao wamekuwa na drama nyingi kwenye tasnia ya muziki huku wasanii wanaotoa muziki mzuri wakisahulika Hata hivyo amedokeza kuachia album yake mwaka huu wa 2022 huku akiwataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea ujio wake mpya ambao ameutaja kama  wakitofauti zaidi.

Read More