DAVIDO AKERWA NA MAPROMOTA WA MUZIKI NCHINI ITALIA

DAVIDO AKERWA NA MAPROMOTA WA MUZIKI NCHINI ITALIA

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Davido ameeleza masikitiko yake kufuatia kutolipwa pesa zake na waandaaji wa tamasha la muziki nchini Italia Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram, kwa uchungu Davido amesema wasanii wanapitia magumu ya kuchosha miili yao kwa jasho na machozi, yote kwa ajili ya mashabiki zao lakini wanaishia kuchukuliwa poa na mapromota. Davido amefunguka kwamba alifika kwenye show hiyo nchini Italia kwa safari ya ndege tatu za kuunganisha, mwisho wa siku promota anashindwa kumlipa pesa zake hadi dakika ya mwisho, licha ya kuuza tiketi takribani Elfu 7. Kwa heshima ya mashabiki zake ambao wamelipa pesa kwa ajili ya kumuona, Davido amesema aliamua kupanda stejini na kufanya show hiyo.

Read More
 DAVIDO NA DABABY WAONEKANA LAGOS KUKAMILISHA COLABO YAO

DAVIDO NA DABABY WAONEKANA LAGOS KUKAMILISHA COLABO YAO

Rapa kutoka Marekani, Dababy ameonekana Nigeria akiwa pamoja na Davido ambaye ndiye kama mwenyeji wake nchini humo. Wawili hao walionekana wakizunguka katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Lagos, huku kila mmoja akishare baadae video wakiwa pamoja kupitia mitandao yao ya kijamii. Aidha, Dababy ametumia ukurasa wake wa Instagram kumshukuru Davido kwa kumfanya ajisikie yupo nyumbani. “Davido amenifanya nijisikie kama nipo nyumbani ”, Ameandika Dababy. Utakumbuka Dababy ametua nchini Nigeria akitokea Ujerumani, ambapo yupo nchini humo kwa ajili ya kukamilisha video ya collabo yake na Davido.

Read More
 DAVIDO ANUNUA KIWANJA CHA SHILLINGI MILLIONI 689 HUKO BANANA ISLAND, NIGERIA

DAVIDO ANUNUA KIWANJA CHA SHILLINGI MILLIONI 689 HUKO BANANA ISLAND, NIGERIA

Mwanamuziki nyota wa Nigeria Davido ametumia zaidi ya shilingi million 689 za Kenya kununua kiwanja katika eneo la kifahari nchini Nigeria, Banana Island. Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Davido amesema amenunua eneo hilo kwa ajili ya kujenga nyumba ya ndoto yake. Davido ambaye ni mkazi wa eneo hilo, anaongeza idadi ya nyumba nyingine Banana Island kwani tayari anamiliki Jumba la kifahari ambalo alilinunua mwaka 2020 kwa zaidi ya shilling million 157 za Kenya.

Read More
 DAVIDO AKAVA JARIDA LA WAVE UINGEREZA

DAVIDO AKAVA JARIDA LA WAVE UINGEREZA

Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido ameendelea kuchana mbuga Kimataifa mara baada ya kutokea kwenye cover la jarida maarufu la burudani nchini Uingereza. Kupitia toleo hili jipya la Jarida hilo, limeangaza maisha ya Davido kwa undani na jinsi alivyofanikiwa na namna alivyoweza kusapoti vipaji vingine nchini humo pasipo kuingiza biashara ndani yake. “Lebo yangu sio biashara, ninatoa fursa kwa sababu kuna watu wengi wenye vipaji nchini Nigeria” amesema Davido akiliambia jarida la Wave Magazine. Mbali na hilo pia amezungumzia juu ya kuendelea kupanua ushawishi wa Kimataifa katika muziki wa Afrobeats.

Read More
 DAVIDO KUGAWA MTAJI WA SHILLINGI MILIONI 5.5 KWA WATU 20 NIGERIA

DAVIDO KUGAWA MTAJI WA SHILLINGI MILIONI 5.5 KWA WATU 20 NIGERIA

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Davido ametangaza habari njema kwa raia nchini humo kuwa ana mpango wa kugawa shillingi Milioni 5 za Kenya kwa watu 20  walio na mawazo ya biashara ili wajikwamue kiuchumi. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Davido ameeleza kwamba anahisi serikali ya Nigeria imeshindwa kusaidia raia wake kukua kiuchumi kwani raia wengi kwa sasa wanategemeana kuinuana kimaisha. Hata hivyo, amewataka raia wa Nigeria kumtumia mawazo ya kibiashara na atachagua washindi ambao atawapa kiasi hicho cha pesa. Kwa mujibu wa taarifa kutoka blogu mbalimbali za Nigeria ni kwamba tayari watu wengi wametoa mawazo yao ya kibiashara kwa mwanamuziki huyo na wanasubiri kuona ikiwa watabahatika. Mpango wa kugawa shilling Milioni 5 za Kenya kwa watu 20 umepangwa kufanyika leo Machi 18.

Read More
 DAVIDO AWACHANA WANAOHUSISHA WATOTO WAKE KWENYE SKENDO ZA KIJINGA

DAVIDO AWACHANA WANAOHUSISHA WATOTO WAKE KWENYE SKENDO ZA KIJINGA

Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido amewatolea uvivu watu wanaopenda kuhusisha familia yake haswa watoto wake kwenye skendo zisizo na msingi kwa kueleza kuwa ni heri wamtaje kwenye skendo hizo badala ya kuwahusisha watoto wake. Davido ameitoa kauli hiyo ambayo alikusudia kumjibu shabiki ambaye alimuambia kupitia mtandao wa twitter kuwa sio Baba halali wa mtoto wake wa kiume “Ifeanyi” ambaye alipata na Chioma. Shabiki huyo alimchana Davido kuwa mtoto huyo baba yake mzazi ni msanii Peruzzi. Ikumbukwe msanii Peruzzi aliwahi kuhusishwa kuwa na mahusiano na Baby Mama huyo wa Davido, mwanadada Chioma.

Read More
 DAVIDO AVUTA NDINGA MPYA YENYE THAMANI YA SHILLINGI MILLIONI 34 ZA KENYA

DAVIDO AVUTA NDINGA MPYA YENYE THAMANI YA SHILLINGI MILLIONI 34 ZA KENYA

Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido anazidi kuongeza list ya magari ya kifahari anayoyamiliki kwenye eneo la kuegesha magari nyumbani kwake mara baada ya kuongeza gari lingine la thamani aina ya Mercedes Maybach GLS 600. Unaambiwa ndinga hiyo mpya aina ya Mercedez Maybach GLS 600 ya Mwaka 2022 inatajwa kuwa na thamani ya $ 300K ambazo ni takribani shilling Milioni 34.2 kwa pesa ya Kenya huku akitarajia kupokea ndinga yake nyingine aina ya Lamborghini itakayotua Nigeria kutoka Dubai.

Read More
 DAVIDO ATOZWA FAINI YA SHILLINGI MILLIONI 42 ZA KENYA KWA KUZIDISHA MUDA O2 ARENA

DAVIDO ATOZWA FAINI YA SHILLINGI MILLIONI 42 ZA KENYA KWA KUZIDISHA MUDA O2 ARENA

Mwanamuziki kutoka Nigeria davido amejikuta akilipa zaidi ya  shilling million 42 za Kenya kama faini baada ya kuzidisha muda katika show yake iliyofanyika juzi kati katika uwanja maarufu nchini uingereza wa O2 Arena. Show ya Davido ilipaswa kuisha saa tano kamili usiku ila msanii huyo alitumbuiza hadi saa  saa tano na dakika 34 huku akisema hajali kuhusu faini hiyo ambayo inasema kuwa kama msanii atazidisha muda wa kutumbuiza atatakiwa kulipa shilling million 1.2 za Kenya kwa kila dakika. Hii si mara ya kwanza kwa wasanii kulipishwa faini hizo kubwa kwani mwaka 2013, Msanii justin bieber alijikuta akilipa faini ya shilling million 37.2 za kenya baada ya kuzidisha dakika 30 kwenye ukumbi huo.

Read More
 DAVIDO AKAMILISHA MCHAKATO WA KUTOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA NIGERIA.

DAVIDO AKAMILISHA MCHAKATO WA KUTOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA NIGERIA.

Mwanamuziki kutoka Nigeria Davido na menejimenti yake wametoa taarifa kwa umma, wamesema ule mchakato wa kusaidia watoto yatima umekamilika ambapo kiasi cha shilllingi million 68 za Kenya zimekabidhiwa kwa vituo 292 vya watoto yatima nchini kwao. Mwezi Novemba mwaka jana Davido alipokea kiasi cha shilling millioni 54 kutoka kwa marafiki zake na wadau ambao walichangisha kupitia mitandao ya kijamii kwenye siku yake ya kuzaliwa. Davido aliahidi kiasi hicho cha fedha atakipeleka kwa watoto yatima na akaongeza shillingi millioni 13 kutoka kwenye mfuko wake, hivyo kukafikisha jumla ya shillingi millioni 68.  

Read More
 DAVIDO NA WIZKID WAZIKA TOFAUTI ZAO BAADA YA KUKUTANA CLUB LAGOS  NA KUKUMBATIANA

DAVIDO NA WIZKID WAZIKA TOFAUTI ZAO BAADA YA KUKUTANA CLUB LAGOS NA KUKUMBATIANA

Wanamuziki wa Nigeria Davido na WizKid ni kama wamemaliza tofauti zao ,mara baada ya kukutana kwenye moja ya club huko jijini Lagos nigeria na kukumbatiana huku wakionekana kuwa na furaha kila mmoja. Wanamuziki hao mara kadhaa wametajwa kuwa kwenye ugomvi, na katika hili wanaongeza idadi ya wanamuziki waliopatana ndani ya mwaka huu baada ya Burna Boy kutangaza kumaliza tofauti zake na Davido. Hata hivyo mashabiki wa muziki nchini Nigeria wameonekana kufurahia hatua ya Davido na Wizkid kumaliza ugomvi wao huku wakiwataka wawili hao kuachia  ngoma ya pamoja.

Read More
 DAVIDO MBIONI KUKAMILISHA COLLABO YAKE NA RAPPER DRAKE KUTOKA MAREKANI

DAVIDO MBIONI KUKAMILISHA COLLABO YAKE NA RAPPER DRAKE KUTOKA MAREKANI

Mwanamuziki nyota kutoka nchini Nigeria Davido amethibitisha uwepo wa collabo yake na rapa kutoka nchini Canada Drake mwaka wa 2022.Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Davido ameshare sehemu ya video akiwa anazungumza na rapa huyo kupitia video call na kusindikiza na ujumbe unao ashiria uwepo wa collabo kati yao ifikapo mwaka wa 2022. Kama collabo hiyo itafanikiwa basi Davido atakuwa msanii wa pili mkubwa kutoka Nigeria kufanya kazi na Drake ikizingatiwa kuwa kipindi cha nyuma alifanya kazi ya pamoja na WizKid kupitia nyimbo kama ‘Closer & One dance’

Read More
 DAVIDO ALAMBA DILI NONO LA KUWA BALOZI WA KAMPUNI YA PUMA

DAVIDO ALAMBA DILI NONO LA KUWA BALOZI WA KAMPUNI YA PUMA

Davido ametangaza kusaini dili nono la kuwa balozi wa kampuni maarufu ya mavazi ya michezo duniani PUMA. Mkali huyo kutoka nchini Nigeria atakuwa na jukumu la kuitangaza kampuni hiyo kwenye soko la Afrika ambalo linakuwa kwa kasi. Kwa mujibu wa ripoti, inaelezwa kuwa Davido pia atakuwa na jukumu la kuitangaza PUMA kwenye eneo la kusini mwa jangwa la Sahara, Amerika ya Kaskazini na dunia kwa ujumla. Davido atakuwa akivaa mavazi ya kampuni hiyo kama miongoni mwa makubaliano yao na pia kufanya matangazo ya michezo kama mpira wa Kikapu na mpira wa Miguu.

Read More