D’Banj akamatwa kwa madai ya utapeli
Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Nigeria (ICPC) imemkamata Mwanamuziki Oladapo Oyebanji almaarufu kama D’Banj kwa madai ya utapeli wa kuchepusha mamilioni ya pesa za mradi wa N-Power. Vyombo vya habari nchini Nigeria vinaripoti kwamba D’Banj amefanya utapeli huo kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali. Mradi wa N-Power ulianzishwa mwaka 2016 na Rais Muhammadu Buhari ambapo lengo kuu ni kusaidia vijana wasio na ajira kwa kuwapatia pesa.
Read More