EP ya Diamond Platnumz “First Of All” yashinda tuzo Marekani
EP ya Diamond Platnumz “First Of All” ama FOA imeshinda tuzo ya album bora ya mwaka 2022 kwenye tuzo za African Entertainment Awards USA (AEAUSA) zilizotolewa usiku wa kuamkia leo huko Marekani. Kwenye tuzo hizo za 8, FOA ilikuwa imeingia kwenye kipengele cha album bora ya mwaka ambapo ilikuwa ikichuana na album nyingine kama “Rave & Roses” ya Rema, “Catch Me If You Can” ya Adenkunle Gold, “Affection” ya Magasco Bboy pamoja na “The Guy” ya Mi Abaga FOA Ep ilitoka rasmi Machi 12, mwaka 2022 ikiwa na jumla ya ngoma 10 huku wanamuziki wanne tu wakiwa wamepewa shavu la kusikika kwenye project hiyo ambao ni Zuchu, Mbosso, Adenkunle Gold na Jaywillz.
Read More