CHRIS BROWN ADAIWA KUPATA MTOTO WA TATU NA MWANAMITINDO DIAMOND BROWN

CHRIS BROWN ADAIWA KUPATA MTOTO WA TATU NA MWANAMITINDO DIAMOND BROWN

Staa wa muziki kutoka nchini Marekani Chris Brown ameripotiwa kuwa amepata mtoto wa tatu na mrembo mwanamitindo aitwaye Diamond Brown ambaye ame-share taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa instagram. Mrembo huyo pia amelitaja jina la mtoto huyo wa Kike kuwa ni Lovely Symphani Brown. Jina la katikati la mtoto ‘Symphani’ limepelekea watu kuhisi Breezy ndio Baba wa mtoto huyo, kwani limefanana na jina la taasisi yake iitwayo Symphonic Love. Chris Brown tayari ana watoto wawili; Aeko Catori Brown mwenye umri wa miaka miwili, pia ana binti mkubwa Royalty mwenye umri wa miaka 8.

Read More
 CHRIS BROWN MBIONI KUPATA MTOTO WA 3 NA EX-GIRLFRIEND WAKE DIAMOND BROWN

CHRIS BROWN MBIONI KUPATA MTOTO WA 3 NA EX-GIRLFRIEND WAKE DIAMOND BROWN

Inatajwa kuwa huenda msanii Chris Brown akawa anatarajia kupata mtoto wake wa tatu, hii ni baada ya ex girlfriend wake mwanamitindo Diamond Brown kuonesha ujauzito wake na kuwa huenda akajifungua siku za hivi karibuni hii ni kwa mujibu wa tovuti ya rapup Bado mwanamitindo huyo hajaweka wazi kama Chris Brown ndiye baba wa mtoto huyo, lakini alithibitisha kuwa ni mjamzito kwa kupost misururu ya picha katika ukurasa wake wa Instagram. Hata hivyo nyota huyo wa RnB Chris Brown hajazungumzia suala hilo mahala popote pale kama ni kweli ama si kweli, lakini kama itakuwa ni kweli basi Breezy atakuwa na jumla ya watoto watatu kutoka kwa wanawake watatu tofauti.

Read More