Diana B Awaacha Mashabiki Midomo Wazi kwa Matumizi ya Nyumbani ya Zaidi ya KES 119,000

Diana B Awaacha Mashabiki Midomo Wazi kwa Matumizi ya Nyumbani ya Zaidi ya KES 119,000

Malkia wa mitandao ya kijamii, Diana B, ameonyesha kwa vitendo namna anavyotumia kwa busara pesa anazozikeshea na kuzitolea jasho kupitia kazi zake mbalimbali. Mkali huyo wa “Bibi ya Tajiri” amewaacha mashabiki wengi vinywa wazi baada ya kufichua kiasi kikubwa cha fedha alichotumia kwa ununuzi wa bidhaa za matumizi ya nyumbani kwa mwezi wa Januari. Kupitia Instastory yake, Diana B ameshare risiti ya manunuzi inayoonyesha alitumia jumla ya KES 119,009 kununua bidhaa mbalimbali za matumizi ya kila siku nyumbani. Hatua hiyo imekuja katika kipindi ambacho Wakenya wengi wanapitia changamoto za kiuchumi, hasa mwezi wa Januari unaojulikana kwa mzigo mkubwa wa karo za shule na mahitaji mengine.

Read More
 Familia ya Bahati Yajiandaa Kumpata Mtoto Mwingine Baada ya Ujauzito Kuthibitishwa

Familia ya Bahati Yajiandaa Kumpata Mtoto Mwingine Baada ya Ujauzito Kuthibitishwa

Malkia wa mitandao ya kijamii na mke wa mwanamuziki Bahati, Diana Marua, amethibitisha rasmi kuwa ni mjamzito, akifunga mjadala na tetesi zilizokuwa zikiendelea kwa kasi mitandaoni. Kupitia video aliyoshiriki, Diana amewaleta watoto wake pamoja kwa mazungumzo kabla ya kuwafahamisha kuwa familia yao iko njiani kumpokea mwanafamilia mpya. Akiwa na tabasamu na msisimko, amewaambia watoto wake kuwa wanatarajia kupata mdogo wao, jambo lililozua furaha na shangwe. Katika mazungumzo hayo, Diana amewauliza watoto wake kama wangependa mdogo wa kiume au wa kike, kauli iliyopokelewa kwa furaha kubwa. Akimgeukia binti yake Malaika, Diana amesisitiza kuwa ujio wa mtoto huyo utaboresha na kubadilisha maisha yao. Kwa sasa, Diana na Bahati wameonesha shukrani zao kwa Mungu na kwa mashabiki wao, wakisema wako tayari kufungua ukurasa mpya wa baraka na furaha katika familia yao inayoendelea kukua.

Read More
 Diana B Awaonya Mabinti Wanaonyemelea Mwanaye Morgan Bahati Mtandaoni

Diana B Awaonya Mabinti Wanaonyemelea Mwanaye Morgan Bahati Mtandaoni

Mwanamitandao aliyegeukia muziki Diana Bahati amemwonya waziwazi mabinti mtandaoni kumuepuka mwanawe, Morgan Bahati, kufuatia mawasiliano ambayo hayakumpendeza kama mzazi. Katika ujumbe wake, Diana amesisitiza kuwa hana tatizo na mashabiki kumpenda au kuwasiliana na Morgan, lakini amekemea vikali tabia ya wasichana kumwomba hela mtoto wake, akibainisha kuwa lengo lake ni kuhakikisha Morgan anazingatia masomo na malezi mema bila shinikizo au ushawishi wa nje. Diana, akiwa na msimamo mkali kuhusu malezi na muda wa watoto wake, ametumia mitandao yake kuwakumbusha mabinti hao kuwa Morgan bado ni mwanafunzi na hana uwezo wala wajibu wa kutoa pesa kwa mtu yeyote kwa sasa. Kauli ya Diana B inakuja mara baada ya binti mmoja kuonekana akimfuata Morgan kupitia mitandao ya kijamii na hata kumwomba pesa.

Read More
 Diana B Amtaka Bahati Afute Wimbo Wake Mpya kwa Sababu za Maadili

Diana B Amtaka Bahati Afute Wimbo Wake Mpya kwa Sababu za Maadili

Mwanamitandao aliyegeukia muziki Diana B amemkosoa hadharani mume wake, Bahati, kufuatia kuachia video ya wimbo wenye utata uitwao “Seti.” Diana amemtaka Bahati kuondoa video hiyo ya wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii, akieleza kuwa maudhui yake hayaendani na maadili ya kifamilia. Amesema kuwa hatakuwa tayari kuendeleza uhusiano wao wa kifamilia hadi pale Bahati atakapochukua hatua hiyo, akimhimiza pia kuwa makini zaidi na maisha badala ya kuendeleza mizozo isiyo ya lazima. Kwa mujibu wa Diana, wasanii wanapaswa kuheshimu taasisi ya ndoa na kuzingatia maadili wanapotayarisha kazi zao za sanaa, kwani jamii huwatazama kama mfano wa kuigwa. Hata hivyo, taarifa zinaonyesha kuwa timu ya YouTube haijaona tatizo lolote katika wimbo huo “Seti,” ambao umeendelea kutazamwa kwa wingi na kuvutia maoni mengi kutoka kwa mashabiki wa muziki wa Bahati.

Read More
 Diana Marua Ajitenga na Mwelekeo Mpya wa Muziki wa Bahati

Diana Marua Ajitenga na Mwelekeo Mpya wa Muziki wa Bahati

Mke wa msanii Bahati, Diana Marua, ameibua gumzo mtandaoni baada ya kujitenga wazi na mwelekeo mpya wa muziki wa mumewe unaohusisha maudhui yanayodaiwa kwenda kinyume na maadili ya jamii. Kupitia taarifa yake kwa mashabiki, Diana amesema anatambua na anaheshimu safari ya Bahati kama msanii na maamuzi anayochukua kwa ajili ya taaluma yake, lakini akasisitiza kuwa mtazamo wake binafsi ni tofauti. Ameeleza kuwa amejikita zaidi katika biashara, ushirikiano wa kibiashara na chapa zinazomwamini, hivyo lazima aendelee kujiwasilisha kwa njia inayoonyesha uwajibikaji, ukuaji na thamani anazoamini. Aidha, Diana ameongeza kuwa kwa heshima ya familia yake, washirika wake kibiashara na wale wanaomchukulia kama kielelezo, hatahusika na mwelekeo ambao Bahati amechukua katika muziki wake. Amesisitiza kuwa anaamini katika kupeana sapoti, lakini pia ni muhimu kulinda chapa yake na nafasi ambazo ameendelea kujenga katika tasnia ya burudani. Diana ametoa kauli hiyo baada ya Bahati kuachia wimbo wake mpya Seti, ujio wake wa kwanza tangu arejee kwenye muziki baada ya mapumziko, ambao hata hivyo umekosolewa vikali kutokana na maudhui yake yanayohamasisha ngono.

Read More
 Diana Bahati Aonyesha Utajiri wake Wakati Mumewe Akikumbwa na Kashfa

Diana Bahati Aonyesha Utajiri wake Wakati Mumewe Akikumbwa na Kashfa

Mke wa msanii Bahati, Diana Marua maarufu kama Diana B, amewajibu kimkakati wanaozidi kumbeza mume wake Bahati ambaye anahusishwa na kashfa ya kushindwa kutimiza ahadi yake ya kutoa KSh1 milioni kwa timu ya taifa, Harambee Stars. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diana alionekana akijivunia shopping ya mwezi mmoja iliyogharimu takribani KSh160,000. Bidhaa alizonunua zilijumuisha vyakula, bidhaa za nyumbani na mahitaji mengine ya familia yake. Hata hivyo, kilichowashangaza wengi ni pale alipoweka wazi wingi wa pesa taslimu alizokuwa nazo nyumbani. Diana alionekana akishika mirundo ya noti za KSh1,000, ambazo alidai zinafikia jumla ya KSh2 milioni. Wakati mashabiki wengine wakivutiwa na maisha ya kifahari anayoyaonesha, wengi walishangaa hatua yake ya kuonyesha kiasi kikubwa cha fedha hadharani, hasa ikizingatiwa kwamba Bahati anatupiwa lawama kwa kukosa kutimiza ahadi yake ya kifedha kwa wachezaji wa Harambee Stars baada ya ushindi wao mkubwa kwenye mashindano ya CHAN 2024. Mashabiki mtandaoni wamehoji uhalisia wa pesa hizo, wengine wakisema huenda ilikuwa njia ya Diana kutafuta kiki na kutetea hadhi ya kifamilia wakati jina la Bahati linatikiswa na shinikizo la mashabiki na wanamichezo.

Read More
 DIANA B AFUNGUKA KUHUSU UKIMYA WA MUME WAKE BAHATI

DIANA B AFUNGUKA KUHUSU UKIMYA WA MUME WAKE BAHATI

Mwanamuziki na mtayarishaji wa maudhui nchini Diana Bahati, amemkingia kifua mumewe Kevin Bahati, kwa madai ya kutotumia akaunti yake ya Instagram kwa muda mrefu. Akimjibu shabiki yake aliyetaka kufahamu kiini cha ukimya wa hitmaker huyo wa ngoma Adhiambo diana b kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema ukimya wa bahati umetokana na msanii huyo kujikita zaidi kwenye masuala ya kifamilia kwani anatumia muda wake mwingi na watoto wake. Hapo awali, Bahati, alikuwa akiwafahamisha mashabiki wake kuhusu matukio yanayotokea kwenye maisha yake, huku akichapisha maudhui mengi kwenye ukurasa wake ndani ya siku moja. Kwa sasa, ukurasa wa Bahati hauna maudhui mapya tangu alipolia hadharani wiki mbili zilizopita kuhusu masaibu yake ya kisiasa, mara baada ya chama cha jubilee kumpokonya tiketiya kuwania ubunge wa mathare kwenye uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu. Tangu wakati huo, mwanamuziki huyo hajachapishaa kitu chochote kipya kwenye mitandao yake ya kijamii akiwaacha mashabiki zake njia panda.

Read More
 DIANA BAHATI AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA CHINI LEBO YA MUZIKI YA DIANA B ENTERTAINMENT

DIANA BAHATI AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA CHINI LEBO YA MUZIKI YA DIANA B ENTERTAINMENT

Mwanamitandao aliyegeukia muziki nchini Diana Bahati amemtambulisha msanii wake mpya wake mpya anayekwenda kwa jina la Vinny fleva. Kupitia ukurasa wake wa instagram Diana B amesema vinny flava atakuwa chini ya lebo yake ya muziki ya Diana B Entertainment ambayo itasimamia kazi zake zote za muziki huku akiwataka mashabiki zake wamkaribishe msanii huyo  ambayo kwa mujibu wake anakuja kubadilisha tasnia ya muziki nchini Kenya. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofauti kimawazo na diana b ambapo wengi wamehoji amemuiga staa wa muziki nchini Nadia Mukami ambaye juzi kati alimtambulisha msanii wake aitwaye Latinoh chini lebo yake ya Sevens Hub Creative. Tayari Diana B ameachia wimbo wake mpya uitwao “Mubaba” ambao amemshirikisha msanii wake vinny fleva. Wimbo huo ni watatu kwa Diana B tangu aanze career yake ya muziki baada ya one day na Tuachana tu ambazo aliziachia mwishoni mwaka wa 2021.

Read More