Trevor Amkingia Kifua Diana B Baada ya Ukosoaji wa “Bibi Ya Tajiri”

Trevor Amkingia Kifua Diana B Baada ya Ukosoaji wa “Bibi Ya Tajiri”

CEO wa Chama cha Content Creators nchini Kenya, Director Trevor amejitokeza na kumkingia kifua Diana B baada ya kupata ukosoaji mkali kutokana na wimbo wake mpya Bibi ya Tajiri ambao una zaidi ya views laki tano youtube ndani ya siku tatu. Hii ni baada ya baadhi ya mashabiki na wakosoaji wa muziki kudai kuwa Diana hana kipaji cha uimbaji na uandishi wa muziki. Akizungumza, Trevor amewataka Wakenya kumuunga mkono Diana badala ya kumbeza, akisisitiza kuwa kila msanii anastahili nafasi ya kujaribu na kukuza sanaa yake. Aidha, amewataka wasanii wa Kenya kushirikiana naye ili kuendeleza muziki wa ndani badala ya kumpuuza. Trevor, hata hivyo, amesisitiza kuwa huu ni mwanzo wa safari ya Diana katika muziki na kwamba anastahili nafasi ya kuthibitisha kipaji chake. Ukosoaji huo ulianza baada ya mashabiki kudai kuwa Bibi ya Tajiri ilikuwa sampled kutoka wimbo maarufu wa marehemu E-Sir, Sare Sare. Haikuishia hapo, baadhi walimlaumu Diana kwa kuchana picha za marapa wakubwa nchini kama Khaligraph Jones na Nyashinski kwenye video yake, wakisema kitendo hicho ni kukosea heshima muziki wa hip hop.

Read More
 Director Trevor Ampongeza Bien kwa Kumlipa Vizuri GenZ Goliath Katika Video Mpya ya Muziki

Director Trevor Ampongeza Bien kwa Kumlipa Vizuri GenZ Goliath Katika Video Mpya ya Muziki

Mkurugenzi Mkuu wa Watayarishaji wa Maudhui ya Kidijitali nchini Kenya, Director Trevor, amemsifu msanii Bien kwa kumuonesha heshima ya hali ya juu Gen Z Goliath kwa kumlipa vizuri na kumhudumia ipasavyo kwa ajili ya kuonekana kwa muda mfupi kwenye video ya muziki. Kupitia mitandao ya kijamii, Director Trevor ameweka wazi kuwa Bien alifuata taratibu zote za kazi kwa kulipa kiwango kamili cha malipo, kugharamia usafiri wa Goliath kwa kutumia gari la kifahari aina ya Toyota LX570, pamoja na malazi ya kiwango cha juu wakati wa kutayarisha video ya wimbo wake mpya “All My Enemies Are Suffering” Hii ni tofauti na matukio ya awali ambapo wasanii na waigizaji chipukizi walilalamika kutolipwa au kupuuzwa baada ya kuchangia mafanikio ya kazi mbalimbali za burudani. Mashabiki wengi wamelipongeza tukio hilo wakisema kuwa ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wakubwa kuonyesha heshima na kuthamini mchango wa vipaji vinavyochipuka. Aidha, hatua hiyo imeibua matumaini kwa vijana wengi kuwa na imani na kazi yao huku wakijua kuwa juhudi zao zinaweza kutambuliwa na kuthaminiwa kikamilifu. Video ya wimbo mpya wa Bien,“All My Enemies Are Suffering” umewavutia wengi si tu kwa ubora wa maudhui bali pia kwa jinsi ulivyowajumuisha majina maarufu kama DJ Shiti na Gen Z Goliath, ambao wameongeza ucheshi na mvuto katika video hiyo.

Read More
 Andrew Kibe Afichua Siri ya DMs za Director Trevor, Akanusha Kuomba Msaada

Andrew Kibe Afichua Siri ya DMs za Director Trevor, Akanusha Kuomba Msaada

Mtangazaji na mwanahabari maarufu Andrew Kibe amevunja ukimya na kujibu madai yanayomhusisha na Director Trevor, akisema kuwa taarifa kwamba aliwahi kumwomba msaada si za kweli. Kibe anasema kwa uwazi kuwa ni Trevor ndiye aliyekuwa akimtafuta mara kwa mara kupitia ujumbe wa moja kwa moja (DMs) alipokuwa Marekani, kipindi ambacho Trevor alikuwa bado kwenye uhusiano na Mungai Eve. Kwa mujibu wa Kibe, Trevor alikuwa akimuomba msaada wa kumsadia kufungua upya ukurasa wake wa Facebook, na sasa anamtaka aweke wazi jumbe hizo kwa umma ili ukweli ujulikane. “Ningependa Trevor aonyeshe jumbe alizoniandikia wakati akinitafuta msaada. Aache kupotosha watu,” alisema Kibe kwa msisitizo. Mbali na hayo, Kibe amemkosoa Trevor kwa kile alichokitaja kama tabia ya kutafuta umaarufu wa haraka (clout) kwa kutumia majina ya watu maarufu. Amemshauri aweke kando drama zisizo na msingi na ajikite kwenye kazi halali zitakazompa heshima na mafanikio ya kweli. Pia, amemwonya kuhusu kuweka mahusiano kwenye mitandao, akisema hatua hiyo huweza kuishia kwa fedheha kama ilivyotokea kwa msanii Mulamwah. Kauli hiyo ya Kibe imejibu shutuma zilizotolewa awali na Trevor, aliyedai kuwa Kibe alimdhalilisha kwa kumuita “mwanaume asiyekuwa na msimamo na aliyekaliwa na mwanamke”, kufuatia kuvunjika kwa mahusiano yake na Mungai Eve. Trevor alisema maneno hayo yalimuumiza kihisia na kudhoofisha heshima yake binafsi. Hata hivyo, Trevor amesema amepitia mengi, lakini kwa sasa amepona kihisia, amejijenga upya, na anaendelea kujiimarisha kimaisha na kitaaluma. Amedai kuwa licha ya changamoto alizopitia, ameibuka kuwa mtu mpya mwenye maono mapya. Mvutano huu kati ya wawili hao maarufu umechochea mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku mashabiki wakiwa wamegawanyika kati ya wanaomuunga mkono Kibe na wale wanaompigia debe Trevor. Wapo wanaosema drama hii ni ya kutafuta kiki, huku wengine wakitaka wahusika waache tofauti zao na wajikite kwenye kazi.

Read More