DJ KHALED ATAJA JINA LA ALBUM YAKE MPYA

DJ KHALED ATAJA JINA LA ALBUM YAKE MPYA

DJ Khaled ametangaza rasmi jina la Album yake mpya ambayo itaingia sokoni hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Khaled amesema Album hiyo ameipa jina la “GOD DID” na ni mahususi kwa ajili ya wanaoamini na wasioamini Mungu. “GOD DID”☝🏽 THE OFFICIAL ALBUM TITLE FOR MY 13TH STUDIO ALBUM COMING SOON I made this album for all the believers and non believers. They didn’t believe in us…do you? 🫵🏽 #GODDID” Ameandika Instagram. Licha ya kututajia jina la album yake mpya, DJ Khaled hajaweka wazi idadi ya nyimbo wala wasanii aliowashirikisha kwenye album yake hiyo ila ni jambo la kusubiriwa. “GOD DID” itakuwa ni Album ya 13 kutoka Studio kwa mtu mzima DJ Khaled ikiifuata ‘Khaled Khaled’ ya mwaka 2021 ambayo ilikuwa na jumla ya mikwaju 20 ya moto.

Read More
 DJ KHALED KUTUNUKIWA NYOTA KWENYE HOLLYWOOD WALK OF FAME

DJ KHALED KUTUNUKIWA NYOTA KWENYE HOLLYWOOD WALK OF FAME

Mtayarishaji wa muziki na Dejaay maarufu kutoka nchini Marekani DJ Khaled ataungana na mastaa wengine wakubwa duniani waliopewa heshima ya kutunukiwa nyota kwenye Hollywood Walk of Fame. Kwa mujibu wa mtandao wa Variety, Khaled atatunukiwa nyota hiyo April 11, mwaka huu. Dj khaled amewahi kushinda tuzo za Grammy mara moja, ni mwandishi wa nyimbo na ni mtayarishaji wa muziki. Ametajwa kuwa atatunukiwa nyota hiyo kutokana na mchango wake mkubwa kwenye tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka 18. Utakumbuka, Hollywood Walk of Fame ni eneo la kutembea kwa miguu kando kando ya majengo katika eneo la Hollywood ambapo nyota za watu waliofanya vyema kwenye upande wa burudani zimewekwa. Walengwa ni wanamuziki, waigizaji, waelekezi wa filamu, watayarishaji wa muziki na filamu na makundi ya waigizaji.

Read More