Size 8 na DJ Mo Wathibitisha Ndoa Yao Imerejea Imara Baada ya Misukosuko

Size 8 na DJ Mo Wathibitisha Ndoa Yao Imerejea Imara Baada ya Misukosuko

Wanandoa maarufu kwenye tasnia ya muziki wa injili, DJ Mo na Size 8, wamefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu kipindi kigumu cha ndoa yao, ambapo walitengana kwa muda wa miezi saba kabla ya kurudiana. Kwenye mahojiano na runinga ya TV 47, DJ Mo  alielezea kuwa licha ya kutengana, walidumisha mawasiliano kwa sababu ya watoto wao na upendo uliobaki kati yao.  “Ni kweli tulitengana kwa miezi saba. Lakini hatukuwahi kufungiana nje kabisa. Nikienda kuwaona watoto nilimwambia ‘nakumiss’, na nikaanza kumkatia tena kama mwanzo,” alisema DJ Mo kwa ucheshi. Size 8 naye alikiri kuwa kipindi hicho kilikuwa kigumu, lakini kilikuwa muhimu kwa ajili ya kutafakari, kusamehe, na kukua kiroho na kihisia. Alieleza kuwa maombi, ushauri wa ndoa, na nia ya dhati ya kulinda familia yao vilichangia sana kwenye maridhiano yao. “Tulihitaji hiyo nafasi. Tulikuwa tumechoka, lakini sasa tunatembea pamoja tena, tukijifunza kila siku,” alisema Size 8. Wawili hao walisisitiza kuwa ndoa si rahisi, lakini kwa mawasiliano, uvumilivu na imani, kila changamoto inaweza kushughulikiwa. Waliwatia moyo wanandoa wengine kuzungumza wazi wanapopitia migogoro badala ya kuficha au kukata tamaa. Wanandoa hao, ambao pia ni watangazaji wa kipindi cha Dine With The Murayas, wamekuwa mfano wa ndoa ya kisasa yenye changamoto lakini pia inayoweza kujengwa upya kwa msingi wa upendo na imani. Mashabiki wao wengi wamepongeza uamuzi wao wa kusimulia safari yao ya ndoa kwa uwazi, wakisema inaleta matumaini kwa wapenzi na wanandoa wengine wanaopitia changamoto kama hizo.

Read More
 SIZE 8 AFUNGUKA KUHUSU MADAI YA KUIKIMBIA NDOA YAKE

SIZE 8 AFUNGUKA KUHUSU MADAI YA KUIKIMBIA NDOA YAKE

Msanii wa nyimbo za injili Size 8 Reborn amethibitisha kwamba ni kweli aliondoka nyumbani kwake baada ya kuingia kwenye ugomvi na mume wake DJ MO. Akizungumza na mashabiki zake mapema leo kupitia channel yake ya Youtube amesema alikuwa amemkasirikia mume wake ambaye alikuwa amemkosoa hivyo alihitaji nafasi ya kukaa pekee yake na kujifikiria. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mateke” amesema anashukuru Mungu wamerudiana pamoja baada kumaliza tofauti zao walipopatanishwa na marafiki pamoja na viongozi wa dini. Katika hatua nyingine msanii huyo ambaye pia ni kasisi ametoa angalizo kwa mashabiki zake kutoharibu ndoa zao kisa migogoro isiyokuwa na msingi huku akiwataka kutafuta ushauri nasaha mahusiano yao yanapoingiwa na ukungu. Utakumbuka wikiendi hii iliyopita taarifa za Size 8 kuikimbia ndoa yake ziligonga vichwa vya habari ambapo alidaiwa kuondoka nyumbani kwake akiwa na watoto wake wawili baada ya mume wake DJ MO kumsaliti.

Read More
 NDOA YA SIZE 8 NA DJ MO YAVUNJIKA

NDOA YA SIZE 8 NA DJ MO YAVUNJIKA

Mitandao mbali mbali ya burudani nchini imeripoti kuwa Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Size 8 Reborn ameikimbia ndoa yake mara baada ya kuingia kwenye ugomvi mkali na mume wake DJ Mo. Vyanzo vya karibu na wawili hao vimesema Size 8 aliondoka nyumbani kwake wiki iliyopita pamoja na watoto wake wawili kutokana na vitendo vya usaliti. Hata hivyo juhudi za marafiki na wanafamilia kuwalewata pamoja wawili hao hazikuzaa matunda kufutia hatua ya Size 8 kuwataka wampe muda wa kufikiria kuhusu hatma ya ndoa yake. Kwa sasa hitmaker huyo wa ngoma ya “Mateke” hamfuati mume wake DJ MO kwenye mitandao ya kijamii huku chanzo cha ndoa yao kuingiwa na ukungu ikiwa haijulikana.

Read More
 RINGTONE AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUTAKA KUZICHAPA NA MUME WA SIZE 8, DJ MO.

RINGTONE AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUTAKA KUZICHAPA NA MUME WA SIZE 8, DJ MO.

Mwanamuziki wa nyimbo za injili ringtone ameshika vichwa vya habari wikiendi hii iliyopita mara baada ya kutaka kuzichapa na DJ Mo ambaye mume wa msaniii mwenzake Size 8. Purukushani  kati ya wawili hao ilianza baada ya ringtone kuzua vurugu kwenye hafla ya uzinduzi wa album ya msanii size 8 ambayo imefanyika Februari 13 mwaka huu kwa kutaka kujiunga na wahubiri waliopewa nafasi ya kuibariki album ya size 8, Christ Revealed kabla ya kuingia sokoni. Sasa suala hilo lilimlazimu mume size 8, DJ MO kutumia nguvu kumuondoa ringtone kwenye eneo la tukio kutokana na msanii huyo kutaka kuaharibu hafla ya uzinduzi wa album size 8 kwa kusisitiza kujiunga na wachungaji kwa lazima. Akizungumza nje ya hafla ya uzinduzi wa album size 8 ringtone amesema ameshangazwa na hatua ya DJ Mo kumkataza kujiunga na wahubiri wenzake stejini kuiombea album huku akimsuta vikali kwa hatua ya kumvunjia heshima mbele ya umma licha ya kuwa msanii mkongwe kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini. Kwa upande wake DJ MO amepuzilia mbali madai ya ringtone kwa kusema kwamba hayana msingi wowote kwani msanii huyo anapenda kuleta mzaha kwenye shughuli za watu hivyo hangemruhusu kuaharibu hafla ya uzinduzi wa album ya mke wake Size 8. Hata hivyo  jambo hilo limezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kwani walimwengu wameonekana kumshambulia  ringtone kwa hatua kuvuruga shughuli ya yenyewe huku wengine wakihoji kuwa huenda msanii huyo anatengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwa ajili ya wimbo wake na size 8 ambao unapatikana kwenye Christ Revealed album

Read More