PRODYUZA WA MUZIKI NCHINI MAVO ON THE BEAT AMCHANA DJ PINYE KWA KUKOSOA MUZIKI WA GENGETONE

PRODYUZA WA MUZIKI NCHINI MAVO ON THE BEAT AMCHANA DJ PINYE KWA KUKOSOA MUZIKI WA GENGETONE

Prodyuza wa muziki nchini Mavo On The Beat DJ amemchana DJ mkongwe Pinye kwa kauli yake aliyotoa kuwa ni vigumu kupiga muziki wa Gengetone kwenye soko la Kimataifa kutokana na muziki huo kukosa ubora. Akipiga stori na Plug TV prodyuza huyo amemsuta vikali DJ Pinye kwa kauli yake hiyo kwa kusema kuwa muda wake umepita na hana usemi kwenye  muziki wa Kenya hivyo aache swala la kuwaingilia wasanii wa Kenya ambao wanatia bidii kwenye kazi zao. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao wa kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na Mavo On The Beat ambapo wamemtaka  prodyuza ajikite kwenye ishu ya kuwashauri wasanii wa gengetone watoe muziki mzuri badala ya kuimba muziki ambao hauna mashiko kwa jamii. Ikumbukwe juzi kati DJ Pinye kwenye mahojiano na Standard Media aliwapa wasanii wa Kenya changamoto kutoa nyimbo zenye ubora ambazo zitapigwa katika mataifa kama Nigeria, Afrika Kusini na mataifa mengine ambayo yanaongoza kimuziki duniani.

Read More
 WASANII WA WAMSHAMBULIA DJ PINYE KWA MADAI YA KUUKOSOA MUZIKI WA KENYA

WASANII WA WAMSHAMBULIA DJ PINYE KWA MADAI YA KUUKOSOA MUZIKI WA KENYA

DJ mkongwe nchini DJ Pinye amejipata pabaya mara ya baada ya wasanii wa muziki nchini kumsuta vikali kwa kauli yake aliyotoa majuzi kuwa ni vigumu kupiga muziki wa Kenya ughaibuini kutokana na muziki huo kukosa ubora ambao unahitajika kimataifa. Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Nairobi Gossip Club wasanii wa Kenya wakiongozwa na Kenrazy wameokana kukasirishwa na kauli hiyo ya DJ Pinye ambapo wamemtaka DJ huyo akome kuwavunjia heshima wa wasanii wa kenya heshima kwa lengo la kujitakia makuu. Kauli ya Kenrazy imetiwa uzito na VDJ Jones pamoja Bien wa Sauti Sol ambao wamesema DJ Pinye muda wake umepita na hana usemi keny  muziki wa Kenya kwani ameishiwa na mawazo ya kufanya kazi yake ya kudeejay ndio maana amehamua kuwaingilia wanamuziki wa kenya ambao wanatia bidii kwenye kazi zao. Ikumbukwe juzi kati DJ Pinye kwenye mahojiano na Standard aliwapa wasanii wa Kenya changamoto kutoa nyimbo zenye ubora ambazo zitapigwa katika mataifa kama Nigeria, Afrika Kusini na mataifa mengine ambayo yanaongoza kimuziki duniani.

Read More