DJ Shiti Atoa Wito kwa Jamii Kumsaidia Yesu wa Tongaren Kugeuza Umaarufu Wake kuwa Fursa ya Maendeleo

DJ Shiti Atoa Wito kwa Jamii Kumsaidia Yesu wa Tongaren Kugeuza Umaarufu Wake kuwa Fursa ya Maendeleo

Mchekeshaji maarufu na mjasiriamali wa burudani, DJ Shiti, ameibua hisia kubwa mitandaoni kwa kutoa wito wa kumsaidia Yesu wa Tongaren, mtu maarufu nchini Kenya ambaye ameijizolea umaarufu kutokana na imani yake ya kipekee ya kiroho. DJ Shiti anasisitiza kwamba kuna haja ya kubadilisha namna ambavyo Yesu wa Tongaren anavyotumika kwenye vyombo vya habari na jamii kwa jumla, ili kumsaidia kutumia umaarufu wake kwa manufaa ya kifedha na maendeleo endelevu. Katika mahojiano ya hivi karibuni, DJ Shiti alisema: “I am willing kumshika mkono, content yake isiende tu ivo, imsaidie.” Kauli hii inaonesha dhamira yake ya kusaidia Yesu wa Tongaren, ambaye ameonekana kwenye vipindi maarufu vya kimataifa, lakini bado ana changamoto ya kutumia umaarufu wake kwa njia inayoweza kumletea kipato cha kudumu. DJ Shiti alielezea masikitiko yake kuhusu namna ambavyo waandishi wa habari na wanaotengeneza maudhui mtandaoni wanavyomshirikisha Yesu wa Tongaren katika makala maalum na vipindi vya runinga, kisha kumuacha bila msaada wowote. “Ni vibaya sana watu wanamhoji na hawamuachii hata ka kitu… ameonekana kwa documentaries kubwa kubwa, and that shows hii kitu gava inafaa ku-consider kama tourist attraction – having Jesus in Kenya,” alisema DJ Shiti kwa msisitizo. Kauli hii inaonyesha kwamba, licha ya umaarufu wa Yesu wa Tongaren, bado serikali na wadau wengine wa sekta ya utalii wamepuuza uwezekano wa kutumia umaarufu wake kama kivutio cha utalii. DJ Shiti aliongeza kwamba ni muhimu kwa jamii ya waandishi wa habari, wasanii, na serikali kuzingatia uwepo wa fursa ya kumsaidia Yesu wa Tongaren kwa njia ya maendeleo endelevu. Alipendekeza kuwa serikali inapaswa kufanya kazi na wadau wa sekta ya utalii na burudani ili kumshirikisha Yesu wa Tongaren kwenye majukwaa rasmi ya utalii, badala ya kumtumia kama kipengele cha vichekesho. Kauli yake imewavutia wengi, huku baadhi ya wafuasi wake wakitaka kuona hatua halisi zikichukuliwa kama vile kumpatia ushauri wa kitaalamu kuhusu maudhui, kuunda jukwaa lake la kidijitali, au hata kutengeneza filamu au vipindi vya runinga vinavyomshirikisha.

Read More
 DJ Shiti afunguka sababu za kutokuwepo kwenye msimu mpya wa Househelps of Kawangware

DJ Shiti afunguka sababu za kutokuwepo kwenye msimu mpya wa Househelps of Kawangware

Kipindi maarufu cha televisheni cha Househelps of Kawangware kimerejea hewani na mashabiki wamegundua kuwa Dj Shiti si miongoni mwa waigizaji walioshirikishwa kwenye msimu mpya wa kipindi hicho. Akizungumza katika mahojiano hivi karibuni, DJ Shiti amesema ameshikika na majukumu mengi ya kikazi nje ya Nairobi kwa kufanya kazi katika miradi tofauti, katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma huko Turkana ambayo huenda iliathiri uwepo wake katika msimu mpya wa Househelps of Kawangware. DJ Shiti hata hivyo ameahidi kwamba atarejea hivi karibuni  kwenye kipindi hicho. “Ni shoo kubwa na mashabiki wangu watarajie kuniona hivi karibuni. Bado nitakuwa Shiti yule yule mzee ambaye hadhira inampenda.”, Alisema. Mchekeshaji huyo amesema anakosa umoja na undugu alioshirikiana na waigizaji wenzake walipokuwa wakifanya kazi pamoja. Househelps of Kawangware ni kipindi ambacho inaangazia maisha ya wafanyakazi wa nyumbani na mwingiliano wao wa kila siku na marafiki wakiwa kwenye harakati zao za maisha.

Read More
 DJ SHITI AMCHANA BABY MAMA WAKE KUPITIA DISS-TRACK “DRAMA ZA MAMA MIRIAM”

DJ SHITI AMCHANA BABY MAMA WAKE KUPITIA DISS-TRACK “DRAMA ZA MAMA MIRIAM”

Mchekeshaji maarufu nchini DJ Shiti ameachIa diss-track iitwayo Drama za Mama Miriam akiwa amemshirikisha Sadii, Diss-track ambayo amemchana baby mama wake ambaye juzi kati alimsuta vikali kwa hatua ya kumtelekeza mtoto wao. Kwenye diss-track hiyo DJ Shiti amesikika kwenye moja ya mashairi akimchana baby mama wake huyo kwa kumtaka aache kumharibia jina ikizingatiwa kuwa kipindi alikuwa amevulia kiuchumi hakuna mtu yeyote alitaka kujihusisha nae. Lakini pia amewachana mablogger na watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaoneza uvumi dhidi yake ambapo amewataka wasiwe wepesi wa kueneza taarifa zisizo kuwa na kweli. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kumubeza dj shiti kwa kuachia diss track kwenda kwa baby wake huyo wakisema mwanaume rijali hana muda ya kujibishana na wanawake huku wengine wakienda mbali zaidi na kuhoji kuwa huenda mchekeshaji huyo anatumia jambo hilo kama kiki ili azungumziwe kwenye vyombo vya habari nchini bada ya kumtambulisha msanii wake Sadii. Utakumbuka wiki iliyopita mwanamke mmoja kwenye mtandao wa Instagram aliibuka kupitia insta story yake na kumtupia DJ Shiti kila aina matusi kwa kumtelekeza mtoto wao kwani amekuwa akituma shillingi 150 kwa ajili ya matunzo.

Read More