Msanii wa zamani wa Jungle Masters Lypso wa Cate afariki dunia

Msanii wa zamani wa Jungle Masters Lypso wa Cate afariki dunia

Aliyekuwa msanii wa Junge Masters Lypso  amefariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 17, 2022 kaunti ya Nairobi. Taarifa hiyo imethibitisha na rafiki yake wa muda mrefu Dogo Richie ambaye amesema msanii huyo alianguka ghafla akiwa bafuni na kufariki papo hapo. Kwa mujibu wa Dogo Richie mipango ya kumpumzisha Lypso kwenye nyumba yake ya milele inaendelea huku akiwataka mashabiki kuiweka familia yake kwa maombi wakati huu mgumu. Lypso ambaye amemuacha mke na mtoto mmoja, enzi za uhai wake aliwahi kutamba na nyimbo kama Size Yangu, Samantha na nyingine nyingi.

Read More
 Dogo Richie asikitishwa na visa vya vijana kujitoa uhai kwa ajili ya mapenzi

Dogo Richie asikitishwa na visa vya vijana kujitoa uhai kwa ajili ya mapenzi

Msanii kutoka Pwani Dogo Richie ametoa ya moyoni kuhusu mabinti wanaotumia mtego wa mapenzi kuwanyanyasa vijana wa kiume kihisia kwa manufaa yao binafsi. Kupitia Whatsapp story yake Hitmaker huyo wa “Tule Sheshe” ametoa changamoto kwa watoto wa kike wasile pesa za wanaume ambao hawana hisia nao kama njia ya kupunguza visa vya vijana kujitoa uhai. Lakini pia amewapa somo vijana wa kiume kwa kuwataka wawakimbie mabinti wanaotumia mahusiano ya kuigiza kama kitega uchumi ya kuwaingizia riziki. Kauli yake imekuja mara baada kijana mmoja ukanda wa Pwani kujitoa uhai kwa madai ya kusalitiwa kimapenzi na mwanadada aliyekuwa anampenda sana.

Read More
 Dogo Richie akiri kwenda kwa mganga kusafisha nyota yake ya muziki

Dogo Richie akiri kwenda kwa mganga kusafisha nyota yake ya muziki

Mwanamuziki kutoka Pwani Dogo Richie kwa mara ya kwanza amekiri kuwa aliwahi kwenda kwa mganga ili amsaidie atoke kimuziki. Katika mahojiano na Presenter Ali Dogo Richie amesema baada ya kufika kwa mganga aliona kuwa hawezi kumsaidia na tangu kipindi hicho aliacha kuamini kwenye masuala ya kishirikina kwani ndio kikwazo kikubwa cha watu wengi kutoendelea kimaisha. Hitmaker huyo wa “Tule Sheshe” amewaasa watu kutoamini katika imani za kishirikina na badala yake wamgeukie Mungu wanapokumbwa na matatizo katika maisha. Lakini pia amenyosha maelezo kuhusu suala la kumtamani kimahusiano malkia wa Tiktok Azziad kwa kusema kuwa ana penzi la kweli kwa mrembo huyo na wala hatafuti kiki kama watu wanavyosema mtandaoni.

Read More
 Dogo Richie atambulishwa Rasmi Kaya Records

Dogo Richie atambulishwa Rasmi Kaya Records

Staa wa muziki nchini, Dogo Richie amepata shavu kubwa baada ya kusainiwa katika lebo ya Kaya Records inayomilikiwa na Kaya Media. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa, Dogo Richie amesema ana furaha tele kujiunga na lebo hiyo huku akiwataka mashabiki zake kusubiri mengi makubwa kutoka kwake kwenye safari yake mpya na Kaya Records. Sanjari na hilo Dogo Richie amesema licha ya kuingia ubia wa kufanya kazi na uongozi mpya, lebo yake ya Reclaim itaendelea na harakati za kuwasaidia vijana kisanaa kwani tayari amewateua watu wapya ambao watasimamia lebo hiyo. Kaya Records ni moja kati ya lebo kubwa sana za muziki ukanda wa Pwani na ilianzisha mwaka 2021 kwa lengo la kukuza vipaji vya vijana kupitia muziki. Utakumbuka kabla ya Dogo Richie kujiunga na Kaya Records,alikuwa anafanya kazi kwa ukaribu na Dallaz Records. Kwa sasa Dogo Richie anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao “Tule Sheshe”, ambao ameuachia chini uongozi wake mpya, Kaya Records.

Read More
 Dogo Richie afunguka sababu ya wasanii wa Kenya kushindwa kutusua kimataifa

Dogo Richie afunguka sababu ya wasanii wa Kenya kushindwa kutusua kimataifa

Mwanamuziki kutoka Pwani Dogo Richie amefunguka sababu za wasanii wa Kenya kushindwa kupenya kwenye soko la kimataifa. Kwenye mkao na waandishi wa habari msanii huyo amesema licha ya wasanii kujikaza kwenye suala la kuachia muziki mzuri, hakuna mazingira rafiki ya kuwawezesha kutanua wigo wa muziki wao kuwafikia wengi kutokana na serikali kutoipa kipau mbele sekta ya muziki ambayo ikipewa uzito huenda ikitangeneza ajira kwa vijana. Dogo Richie ambaye anahisiwa huenda akaingia ubia wa kufanya kazi na Kaya Records, ametangaza kuwa Jumamosi hii ana jambo lake ambapo amewataka mashabiki wamfuatilia kwa ukaribu kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kufahamu na kupokea matukio yote kutoka kwake.

Read More
 DOGO RICHIE AKIRI KUTESWA NA MAPENZI

DOGO RICHIE AKIRI KUTESWA NA MAPENZI

Msanii kutoka Pwani Dogo Richie ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba hajawahi mpata mwanamke anayempenda anavyostahili. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Dogo Richie amesema imekuwa vigumu kwake kupata mwanamke wa ndoto yake kutokana na kazi yake ya muziki. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Hae” amesema sababu kubwa ni kuumiza kimapenzi na pia brandy yake ya muziki ambayo imewavutia wanawake wasiokuwa na malengo nae. Hajafahamika ni kitu gani kimempelekea dogo richie kutoa kauli hiyo ikizingatiwa kuwa kipindi cha nyuma alikiri  kuwa yupo kwenye mahusiano na mrembo wa kikalenjin aitwaye Mercy ambaye alidokeza kuwa ana mpango wa kufanga nae ndoa hivi karibuni.

Read More
 DOGO RICHIE MBIONI KUACHIA EP KABLA YA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA

DOGO RICHIE MBIONI KUACHIA EP KABLA YA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa muziki kutoka Kenya Dogo Richie ametangaza ujio wa EP yake mpya ambayo ni ya kwanza tangu aanze safari yake ya muziki. Katika mahojiano na kipindi cha Interact Extra cha North Rift Radio Dogo Richie amesema Ep hiyo yenye jumla ya ngoma 8  za moto imekamilika kwa asilimia 100 na itaingia sokoni kabla ya ujio wa album yake mpya mwaka huu. Licha ya kutoweka wazi jina na wasanii aliowashirikisha kwenye EP yake mpya, Dogo Richie amewataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kuipokea EP yake hiyo ambayo kwa mujibu wake itakuwa na ladhaa ya kitofauti sana itakayokata kiu ya wafuasi wa muziki wake. Utakumbuka Dogo Richie alipaswa kuachia album yake mpya mwaka 2020 lakini ilishindikana kutokana na janga la korona kusambaratisha baadhi ya mipango yake, jambo ambalo lilimpelekea kuahirisha mchakato mzima wa kuachia album hiyo.

Read More
 DOGO RICHIE AWACHANA MAPROMOTA WA MUZIKI NCHINI KENYA

DOGO RICHIE AWACHANA MAPROMOTA WA MUZIKI NCHINI KENYA

Msanii wa muziki nchini Dogo Richie amedai kuwa waandaaji wa matamasha ya muziki nchini Kenya wamekuwa na tabia ya kuwa dhulumu wasanii kutokana na wao kukosa elimu kuhusu mikataba Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Dogo Richie amesema wandaaji wengine wa tamasha wamekuwa wakiwabadilishia malipo wasanii baada ya kutumbiza kwenye tamasha kwa kutoa sababu zisizo kuwa na msingi wowote. Lakini pia amewalaumu baadhi ya wasaani ambao amesema wamekuwa na hulka ya kuingia mikataba na mapromoter hao kwa njia ya kishikaji, jambo ambalo limepelekea wanamuziki wengi nchini kudharauliwa kwenye shows. Hata hiyo Dogo Richie ambaye kwa sasa anafanya poa na ngoma yake iitwayo “Hae” amesema atahakikisha kuwa makubaliano yote kati yake na promoter yeyote yana nakiliwa kama njia ya kuepuka kutapeliwa.

Read More
 DOGO RICHIE ATOA CHANGAMOTO KWA WASANII WA KENYA KUWA WABUNIFU WA KUTENGENEZA MATUKIO

DOGO RICHIE ATOA CHANGAMOTO KWA WASANII WA KENYA KUWA WABUNIFU WA KUTENGENEZA MATUKIO

Mwanamuziki kutoka Kenya Dogo Richie amesema wasanii nchini humo wanawapa Bloggers wakati mgumu kwa kukosa  ubunifu na kupanga matukio yatakayo wapa nafasi ya kuzungumziwa katika mitandao ya kijamii. Kwenye mahojiano ya hivi karibuni Ndogo Richie amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya mashabiki wengi wa mziki hapa nchini kupenda kusoma tarifaa za burudani katika mitandao ya Udaku ya nchini Tanzania. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Bilnaden” amesema kuwa kwa sasa ni vigumu kwa msanii kupata mafanikio makubwa pasi na kuwa na matukio yatakao mfanya awe gumzo kwa mashabiki zake. Hata hivyo amewapa changamoto wasaani kuwa wabunifu ili kuwapa bloggers maudhui ya burudani yatakayo jenga gumzo kwa mashabiki wao

Read More