Tems, Doja Cat na J Balvin Kuwasha Jukwaa la Club World Cup Usiku Huu

Tems, Doja Cat na J Balvin Kuwasha Jukwaa la Club World Cup Usiku Huu

Usiku wa leo, majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki, macho na masikio ya mashabiki wa soka duniani yatakuwa yameelekezwa kwenye Uwanja wa MetLife, New Jersey, Marekani, ambako fainali ya FIFA Club World Cup itapigwa kati ya mabingwa wa Ulaya, Chelsea FC kutoka England, na mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain (PSG). Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kusisimua na wa kiwango cha juu, ukiwa ndio hitimisho la mashindano hayo ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu. Katika kilele cha tukio hilo, kutakuwa na Halftime Show ya aina yake, ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano ya Club World Cup, kutafanyika onesho la burudani kipindi cha mapumziko. Wasanii watatu wakubwa duniani, Doja Cat kutoka Marekani, J Balvin kutoka Colombia, na Tems kutoka Nigeria watatumbuiza mbele ya mashabiki lukuki ndani ya uwanja na wale wanaotazama kupitia runinga duniani kote. Tukio hili la kihistoria linaashiria hatua mpya katika kuunganisha michezo na burudani, na linathibitisha hadhi ya soka kama jukwaa pana la utamaduni wa dunia.

Read More
 DOJA CAT MBIONI KUWABARIKI MASHABIKI NA ALBUM MPYA

DOJA CAT MBIONI KUWABARIKI MASHABIKI NA ALBUM MPYA

Mwanamuziki kutoka Marekani Doja Cat ametangaza ujio wa album yake mpya ambayo itakuwa kwenye muundo wa R&B na hato-rap kama alivyozoeleka. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameongeza kwa kusema “Sifanyi album ya kitamaduni za kijerumani…nilikuwa nikitania chombo kimoja cha habari ambacho kilinihoji kuihusu”. Hii itakuwa album yake ya nne kutoka studio baada ya kutamba na Amala ya mwaka 2018, Hot Pink ya mwaka 2019 na Planet Her ya mwaka 2021. Kabla ya hapo aliwahi kuachia EP mbili ambazo ni Purrr ya mwaka 2014 na Streets Remixes ya mwaka 2021.

Read More
 DOJA CAT ASITISHA ZIARA YAKE YA MUZIKI KISA UPASUAJI WA KUONDOA TONSIL

DOJA CAT ASITISHA ZIARA YAKE YA MUZIKI KISA UPASUAJI WA KUONDOA TONSIL

Mwanamuziki kutoka Marekani Doja Cat amesitisha ziara yake ya muziki kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa tonsil. Hii ni baada ya mrembo huyo kunywa pombe wakati akiwa kwenye matumizi ya dawa zinazozuia bakteria “antibiotiki” Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe unaosomeka “hi guys nilitamani sana, nilitaka msikie kutoka kwangu kwanza, kwa bahati mbaya natakiwa kufanya upasuaji wa kuondoa tonsil kwa haraka sana.”, Doja Cat Amendika kupitia Instastory yake. Doja Cat ameendelea kwa kusema kwamba “upasuaji tayari umeshapangwa lakini kupona itachukua muda kidogo, kwasababu ya uvimbe. hii ina maana kwamba natakiwa kusitisha tamasha langu katika kipindi hiki cha msimu wa majira ya joto pamoja na ziara ya theweeknd iitwayo “after hours til dawn”. najiskia vibaya juu ya hili lakin ni lazima nisubiri hili nipone niweze kurejea katika hali yangu ili nitengeneze muziki kwajili yenu wote”, Doja Cat Amesisitiza. Hii ina maana kwamba Doja Cat hatotokea kwenye tamasha la Hangout mjini Alabama alilokuwa alifanye wikiendi hii pamoja na Glastonbury huko United Kingdom (uk) alilotakiwa kulifanya mwezi Juni mwaka huu.

Read More