50 Cent Apinga Uwezekano wa Trump Kumsamehe Diddy

50 Cent Apinga Uwezekano wa Trump Kumsamehe Diddy

Rapa maarufu 50 Cent amejitokeza waziwazi kupinga kauli ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu uwezekano wa kumsamehe Sean “Diddy” Combs, ambaye anakabiliwa na mashtaka mazito ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono na uhalifu wa kupanga. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, 50 Cent alionyesha kutoridhishwa na kauli ya Trump, akieleza kuwa Diddy amekuwa akiongea vibaya kuhusu Trump kwa muda mrefu, na hivyo si sahihi kwa kiongozi huyo wa zamani kufikiria kumsamehe mtu ambaye hakumuunga mkono.  “Alisema mambo mabaya sana kuhusu Trump, sio sawa. Nitawasiliana naye ili ajue jinsi ninavyohisi kuhusu mtu huyu.”  aliandika Instagram Kauli hii ya 50 Cent inakuja baada ya Trump kusema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba hajapokea ombi rasmi la msamaha kwa Diddy, lakini yuko tayari kuangalia ukweli wa kesi hiyo kabla ya kufanya uamuzi wowote. Diddy anakabiliwa na mashtaka mazito ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, njama ya uhalifu, na usafirishaji kwa ajili ya ukahaba.  Iwapo atapatikana na hatia, anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Uhusiano kati ya 50 Cent na Diddy umekuwa na mvutano kwa muda mrefu, na 50 Cent amekuwa akitoa maoni ya ukosoaji dhidi ya Diddy mara kwa mara.  Kauli yake ya sasa inaonyesha nia ya kuzuia msamaha wowote kutoka kwa Trump kwa Diddy.

Read More
 NBA YoungBoy Afutiwa Makosa na Trump, Asema: ‘Ni Mwanzo Mpya wa Maisha’

NBA YoungBoy Afutiwa Makosa na Trump, Asema: ‘Ni Mwanzo Mpya wa Maisha’

Rapa maarufu wa Marekani NBA YoungBoy amemshukuru Rais wa Marekani, Donald Trump, kwa kumpa msamaha wa kisheria unaofuta rekodi za makosa ya jinai na kumpa nafasi mpya ya kisheria na kijamii. Kupitia ujumbe wa hadharani alioutoa hivi karibuni, YoungBoy, alieleza shukrani zake kwa hatua hiyo ya Trump, akisema kwamba imekuwa mwanga mpya katika maisha yake na itamuwezesha kuendelea mbele bila mzigo wa kihistoria wa makosa ya zamani. “Nashukuru kwa msamaha huu. Ni mwanzo mpya, na nitautumia vizuri,” alisema YoungBoy. Msamaha huu kwa YoungBoy umetafsiriwa na mashabiki kama njia ya kuufungua ukurasa mpya katika maisha yake. Rapa huyo ambaye amepitia changamoto mbalimbali za kisheria, sasa ana nafasi ya kuimarisha maisha yake binafsi na kazi yake ya muziki bila kuandamwa na rekodi ya makosa ya awali. Hata hivyo, hatua hiyo pia imezua mjadala. Wengine wanasema msamaha kwa watu maarufu huonyesha upendeleo, huku wengine wakisisitiza kwamba kila mtu anastahili nafasi ya pili, hasa pale wanapoonyesha mabadiliko ya kweli. Kwa sasa, mashabiki wa YoungBoy wanasubiri kuona ikiwa msamaha huu utakuwa mwanzo wa awamu mpya ya muziki safi, maisha bila migogoro ya kisheria, na ushawishi chanya kwa vijana.

Read More