Donjo Maber: Wimbo Mpya wa Iyanii na Dufla Wateka Mitandao kwa Midundo ya Afro-Dancehall

Donjo Maber: Wimbo Mpya wa Iyanii na Dufla Wateka Mitandao kwa Midundo ya Afro-Dancehall

Wimbo mpya “Donjo Maber” wa wasanii wa Kenya Iyanii na Dufla Diligon unaendelea kutikisa mitandao ya kijamii na kuchezwa sana kwenye vituo vya redio. Donjo Maber, ni msemo wa jamii ya Luo unaomaanisha jambo limeweza au limetiki, kwenye hii single umetumika kama kauli ya ushindi na vibe nzuri mitaani. Wimbo huu ambao ni moja kati ya single itakayopatikana kwenye Album mpya ijayo ya Iyanii, unachanganya midundo ya Afrobeat na dancehall kwa ustadi mkubwa. Vocals za Dufla zinabeba hisia za mitaani huku Iyanii akitamba na uchezaji wa maneno unaonata. Beat ni kali na mashairi ni mepesi, yanayokaririka kirahisi, jambo ambalo limeufanya kuwa maarufu mitandaoni hasa kupitia #DonjoMaberChallenge kwenye TikTok na Instagram. Video rasmi ni ya rangi kali, nguo za kuvutia na densi zilizopangwa kitaalam. Ingawa haina hadithi nzito, inalenga vibe ya kusherehekea, jambo linaloifanya kuwavutia sana vijana. Tayari ndani ya siku 10 imevuma YouTube ikiwa na zaidi ya views laki 3 huku ikishikilia nafasi ya 6 kwenye trending tab nchini Kenya. Kwa ujumla, Donjo Maber ni ushahidi kuwa muziki wa Kenya unaendelea kukua na kuchukua nafasi katika soko la Afrika na dunia. Ushirikiano kati ya Iyanii na Dufla umeleta ladha ya kipekee ambayo inakonga nyoyo za mashabiki. Ni wimbo wa kujivunia, wa kufurahia, na bila shaka, una nafasi kubwa kuwa hitsong ya mwaka.

Read More