Dr. Dre yupo mbioni kuuza haki za nyimbo zake (Master Recording)

Dr. Dre yupo mbioni kuuza haki za nyimbo zake (Master Recording)

Rapa mkongwe na mtayarishaji wa muziki kutoka Marekani, Dr. Dre ameripotiwa kuwa yupo mbioni kuuza baadhi ya haki za nyimbo zake (Master Recording) kwa Kampuni ya Universal Music Group (UMG) pamoja na Kampuni ya Kimarekani ya Shamrock Holdings. Hata hivyo taarifa za ndani zaidi zinadai, Dr. Dre anauza haki za nyimbo zake zote toka katika LP yake ya kwanza iitwayo “The Chronic” iliyotoka mwaka 1992 pamoja na baadhi ya mirabaha katika utayarishaji na uandishi wa nyimbo zake akiwa na rapa Kendrick Lamar.

Read More
 Rapa 50 Cent adokeza ujio wa ngoma mpya na mtayarishaji nguli Dr. Dre

Rapa 50 Cent adokeza ujio wa ngoma mpya na mtayarishaji nguli Dr. Dre

Baada ya hivi karibuni kudokeza kuwa anafanyia kazi ujio mpya wa kazi zake za muziki kwa mwaka 2023, Rapa 50 Cent ametusanua kuhusu ujio wa ngoma mpya na mtayarishaji nguli Dr. Dre. Kwenye mahojiano na mtangazaji Big Boy, 50 Cent amekaririwa hapo akisema tutarajie ushirikiano wao tena kwa mara nyingine kwani baada ya kutangaza kurudi kwenye muziki alipokea ujumbe mfupi kutoka kwa Eminem ambao ulisema, Dr. Dre ana midundo kwa ajili yake. Ujio wa 50 Cent kwenye dunia ya muziki miaka 20 iliyopita ilifanikishwa na kazi kubwa ya Mtayarishaji Dr. Dre ambaye alipika midundo mizito iliyoweza kunata vyema kwenye mistari ya Rapa huyo ambaye alishikwa mkono na Eminem.

Read More
 Snoop Dogg athibitisha ujio wa Album yake mpya, Adai Dr. Dre amehusika pakubwa

Snoop Dogg athibitisha ujio wa Album yake mpya, Adai Dr. Dre amehusika pakubwa

Mkali wa muziki wa Hiphop Duniani Snoop Dogg amethibitisha ujio wa Album yake mpya “Missionary” ambayo imetayarishwa na swahiba wake wa muda mrefu, Mtayarishaji mkongwe Dr. Dre. Snoop amefunguka hayo kupitia podcast ya ‘Know Mercy’ na Mtangazaji Stephen A. Smith, ambapo amesema Album hiyo ipo jikoni inapikwa kwa sasa. Kwa mujibu wa Snoop ‘Missionary’ itatoka chini ya Death Row Records/Aftermath Entertainment. Album ya kwanza ya Snoop Dogg ilikuwa inaitwa ‘Doggystyle’ na ilitoka November mwaka 1993 ikitengenezwa na Dr. Dre.

Read More
 THE GAME NA TIMU YAKE WAKASIRIKA, WAHOJI NI KWANINI DR. DRE ALIMCHAGUA 50 CENT KWENYE SUPER BOWL 2022

THE GAME NA TIMU YAKE WAKASIRIKA, WAHOJI NI KWANINI DR. DRE ALIMCHAGUA 50 CENT KWENYE SUPER BOWL 2022

Stori kubwa wiki hii kwenye burudani ni Super Bowl Half Time Show ambayo inatajwa kuwa ya kihistoria, lakini The Game ana malalamiko yake. Baada ya 50 Cent kupandishwa na kutumbuiza kama Guest Artist, Rapa The Game pamoja na timu yake wameonekana kutopenda uamuzi huo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, The Game ame-share ujumbe uliowekwa na miongoni mwa memba kwenye timu yake, ambao unasema inakuaje wanampa 50 Cent hiyo nafasi na sio The Game? Game alistahili kuwepo kwenye Jukwaa hilo pia Kauli ya The Game imekuja mara baada ya Super Bowl 2022 Halftime Show kufunguliwa kwa perfomance ya Dr. Dre na Snoop Dogg kupitia ngoma ya “The Next Episode” na “California Love” ya Tupac Shakur, ambapo Rapa na mfanyabiashara 50 Cent alitokea kwenye dakika ya 3:10 kupiga performance ya kufa mtu na ngoma ya “In Da Club” na kuamsha shangwe la aina yake. Eminem ndiye alimpa mashavu 50 Cent kutumbuiza kwenye halftime ya Super Bowl 2022. Eminem ndiye alitoa wazo hilo na kupitishwa na Dre pamoja na wote ambao walikuwa kwenye orodha ya watumbuizaji rasmi. Ikumbukwe Mtayarishaji mkongwe  kutoka Marekani Dr. Dre alitumia shillingi millioni 795 za Kenya kwa ajili ya kutayarisha performance nzima ya Halftime kwenye fainali za Super Bowl 2022 zilizofanyika Februari 14 katika uga wa SoFi huko California. Dunia ilishuhudia Dr. Dre akiandika historia akiwa na wakali wa Hip Hop nchini Marekani; kama Kendrick Lamar, Snoop Dogg, Eminem, 50 Cent na mwanadada Mary J Bridge.

Read More
 DR. DRE ATUMIA PESA ZAKE ZAIDI YA MILLIONI 795 ZA KENYA KUANDAA HALF TIME YA SUPER BOWL 2022

DR. DRE ATUMIA PESA ZAKE ZAIDI YA MILLIONI 795 ZA KENYA KUANDAA HALF TIME YA SUPER BOWL 2022

Mtayarishaji mkongwe  kutoka Marekani Dr. Dre ameripotiwa kutumia shillingi millioni 795 za Kenya kwa ajili ya kutayarisha performance nzima ya Halftime kwenye fainali za Super Bowl 2022 zilizofanyika Februari 14 katika uga wa SoFi huko California. Dunia imeshuhudia Dr. Dre akiandika historia akiwa na wakali wa Hip Hop nchini Marekani; kama Kendrick Lamar, Snoop Dogg, Eminem, 50 Cent na mwanadada Mary J Bridge. Kama ambavyo tunafahamu, NFL huwa haigharamii chochote kwenye performance za wasanii ambao hutumbuiza kwenye Halftime ya fainali za Super Bowl. Mwaka jana mwimbaji The Weeknd alitumia takribani billion moja za Kenya kuandaa onesho lake zima lililokuwa na wanenguaji lukuk

Read More
 DR. DRE AFIKISHIWA NYARAKA ZA TALAKA AKIWA MAKABURINI.

DR. DRE AFIKISHIWA NYARAKA ZA TALAKA AKIWA MAKABURINI.

Sakata la kuvunjika kwa ndoa ya mtayarishaji mkongwe Dr. Dre bado linashika vichwa vya habari duniani, Sasa jipya limeibuka ambapo tovuti ya TMZ imeripoti kwamba Dre amefikishiwa nyaraka za kisheria kuhusiana na mchakato wa talaka, lakini amefikishiwa nyaraka hizo akiwa makaburini. Tunaambiwa Dr. Dre alikuwa akimzika Bibi yake ndipo mtu mmoja alipofika na karatasi hizo kisha kumshikisha Dre ambaye alikuwa amesimama kando ya Jeneza. Taarifa zinasema Dre alikasirika kuona kitendo kama hicho. Tovuti ya TMZ imebaini nyaraka hizo ambazo zilifikishwa kwa Dre zilikuwa zinahusu malipo ya mwanasheria wa aliyekuwa mke wake Bi. Nicole Young kwa ajili ya mchakato huo wa talaka. Kuna mgogoro wa malipo hayo ambapo Dre alilipa takriban shilling million 36.1 badala ya shilling millioni 175 ambayo inadaiwa kwamba Jaji alipitisha akimtaka Dr. Dre ailipe, hivyo karatasi hizo ni agizo la Jaji.

Read More