Dr. Hilderman atangaza ujio wa Album yake mpya

Dr. Hilderman atangaza ujio wa Album yake mpya

Mwanamuziki aliyegeukia siasa kutoka Uganda Dr. Hilderman ametangaza ujio wa Album yake mpya ambayo kwa mujibu wake huenda ikaingia sokoni hivi karibuni. Kupitia mitandao yake ya kijamii Hilderman amesema Album hiyo ambayo ameipa jina la Favor ina jumla ya ngoma 12 ambazo amezichagua kutoka kwenye maktaba yake ya nyimbo 25 alizozirekodi kwa muda wa miaka miwili. Licha ya kutoweka wazi wasanii aliowashirikisha kwenye Album yake mpya, Hilderman amesema Album hiyo imekamilika kwa asilimia 100 ambapo amewataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kuipokea kazi hiyo ambayo kwa amehoji kuwa itakuwa ya kitofauti sana kwenye safari yake ya muziki.

Read More
 Dr. Hilderman aibiwa vifaa vya studio na prodyuza

Dr. Hilderman aibiwa vifaa vya studio na prodyuza

Msanii aliyegeukia siasa kutoka Uganda Dr. Hilderman amejipata akiwa katika hali ya majonzi baada ya prodyuza aliyekuwa amemuajiri kwenye studio zake za Wokota kukimbia na vifaa vyote vya muziki. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Uganda, prodyuza huyo anayefahamika kama Drainer Beats alitekeleza kitendo hicho cha wizi wa mabavu na kisha akazima simu yake ya mawasiliano. Hata hivyo jeshi la polisi nchini humo limeanzisha msako wa kumtafuta mtuhumiwa huku chanzo cha prodyuza kutoroka na vifaa vya studio ikiwa hajawekwa wazi. Ikumbukwe mwezi Oktoba mwaka 2022 Dr. Hilderman alianzisha studios za Wokota kwa nia ya kukuza na kuinua vipaji vya vijana kwenye muziki lakini inaonekana ndoto yake hiyo imekatizwa ghafla na prodyuza Drainer Beats ambaye amemuacha akikadiria hasara ya mamilioni ya fedha.

Read More