Dr. Ofweneke apata kigugumizi baada ya kuitishwa millioni 70 kumleta Burna Boy Kenya

Dr. Ofweneke apata kigugumizi baada ya kuitishwa millioni 70 kumleta Burna Boy Kenya

Mchekeshaji Dr. Ofweneke ameshangazwa na kiasi cha pesa alichotakiwa kulipa kwa ajili ya kumleta Burna Boy kutumbuiza nchini Kenya. Kupitia ukurasa wa Instagram Ofweneke amesema uongozi wa Burna Boy kupitia mama yake mzazi Bose Ogulu ulimtaka alipe kiasi cha shillingi millioni 70 kumpata msanii huyo kutumbuiza kwenye mkesha wa kukaribisha mwaka mpya wa 2023. “Weeh tried reaching out to the mum for a new year’s event … he is now charging Ksh 70 M,” alisema Dr. Ofweneke. Hata hivyo kauli hiyo imezua mjadala mzito miongoni watumiaji wa mitandao ya kijamii wengi wakitamtaka mchekeshaji huyo kuwapa nafasi wasanii wa Kenya kwenye onesho lake lijalo badala ya kuwazingatiwa wasanii wa nje ambao watamtoza kiasi kikubwa cha pesa.

Read More
 DR. OFWENEKE AKANUSHA KUWA KWENYE UGOMVI NA AKOTHEE

DR. OFWENEKE AKANUSHA KUWA KWENYE UGOMVI NA AKOTHEE

Mchekeshaji Dr. Ofweneke amekanusha kuwa kwenye bifu na Akothee baada ya kumtaka mwimbaji huyo amlipe shilllingi millioni 1.4 ili awe mshereheshaji(MC) kwenye hafla ya harusi yake. Kwenye mahojiano na Mpasho Ofweneke amesema hana ugomvi na mwanamama huyo wa watoto 5 kama namna watu wanavyohoji kwenye mitandao ya kijamii kwani ni marafiki wakubwa. Mchekeshaji huyo amesema ana imani kuwa Akothee ana uwezo mkubwa wa kumlipa pesa hizo kwani bado wapo kwenye mchakato wa kukamilisha mazungumzo kati yao.

Read More