Dr. Dre afunguka sababu za kumtetea Kendrick Lamar kwenye bifu na Drake

Dr. Dre afunguka sababu za kumtetea Kendrick Lamar kwenye bifu na Drake

Mtayarishi mkongwe wa muziki nchini Marekani Dr. Dre, amefunguka sababu za kuchagua upande kwenye bifu ya Drake na Kendrick Lamar iliyotikisa ulimwengu wa muziki wa Hiphop duniani. Akizungumza kwenye podcast ya The Unusual Suspects With Kenya Barris and Malcolm Gladwell, Dr. Dre ameeleza kuwa hakuvutiwa na hatua ya Drake kumshambulia Kendrick Lamar pamoja na familia yake. “Ninapenda wimbo wa  ‘Not Like Us’. Lakini niliposikia Drake akisema mambo mabaya kuhusu mke wa Kendrick na watoto wake, nikasema ‘Ah, adios!’”, Alisema Dre. Kauli ya Dr. Dre inakuja muda mfupi baada ya Drake kufungua kesi dhidi ya Universal Music Group kuhusu wimbo ‘Not Like Us’, ambao una mashambulizi makali dhidi yake. Hii si mara ya kwanza Dre kuzungumzia ‘Not Like Us’. Novemba mwaka jana, aliusifu wimbo huo kwa kusema kuwa umeleta mshikamano mkubwa kwa muziki wa Hiphop nchini Marekani.

Read More
 DR. DRE KUMLIPA EX WAKE ZAIDI YA BILLIONI 11

DR. DRE KUMLIPA EX WAKE ZAIDI YA BILLIONI 11

Mahakama imemuamuru mtayarishaji nguli wa muziki duniani Dr. Dre kumlipa aliyekuwa mke wake Nicole Young zaidi ya Shilingi bilioni 11za Kenya baada ya kuvunjika kwa ndoa yao Kwa mujibu wa Tmz Dr Dre anatakiwa kuanza kulipa kiwango nusu cha pesa hiyo na nyingine kumalizia ndani ya mwaka mmoja. Hapo awali Nicole Young alitaka agawane mali nusu kwa nusu na mtayarishaji huyo wa muziki lakini mahakama imetengua hilo na kuamuru Dre kulipa kiasi hicho cha pesa. Nicole atatakiwa kulipa mwenyewe gharama za kuendesha kesi ambazo zinatajwa kuwa mabilioni ya pesa. Dr Dre na Nicole Young ambao wamedumu kwenye ndoa kwa miaka 25, tayari wameshapeana talaka

Read More